Putin aagiza wanadiplomasia 755 wa Marekani kuondoka Urusi Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter HakiAFPImageKufukuzwa wa wanadiplomasia hao kutapunguza idadi hadi 455 Rais wa Urusi Vladimir Putin ameagiza wafanyakazi 755 wa ubalozi wa Marekani nchini Urusi kusitisha shughuli zao kufikia Septemba mosi mwaka huu. Urusi imeidhinisha hatua hiyo kwa ghadhabu kufuatia vikwazo vipya vilivyopitishwa na bunge la Marekani dhidi yake, kwa tuhuma za kuingilia uchaguzi wa taifa hilo mwaka jana. Marekani kwa upande wake, inasema imesikitishwa na uamuzi huo, na inapima athari na kutafakari namna ya kujibu hatua hiyo Marekani yawafukuza wanadiplomasia 35 wa Urusi Bunge la wawakilishi Marekani launga mkono vikwazo dhidi ya Urusi Hatua hii ya Urusi imekuja baada ya vikwazo vipya dhidi ya Urusi kuidhinishwa kwa wingi wa kura na mabunge yote ya congress nchini Marekani Jumanne, licha ya kwamba Ikulu ya White house ilipinga kura hiyo. Rais huyo ...
Usipitwe na Habari za Kila Kona ya Dunia.