Skip to main content

Posts

Showing posts with the label HabariTz

Babu Tale Anakabiliwa na Kesi ya Madai ya Mil 250

Mkurugenzi wa Tip Top Connection Hamis Taletale a.k.a Babu Tale ameachiwa huru toka Kituo Kikuu cha Polisi DSM. Tale anakabiliwa na kesi ya madai ya fidia ya shilingi milioni 250 baada ya kushtakiwa kwa kosa la kutumia kazi ya Mhadhiri Sheikh Hashim Mbonde bila ridhaa yake. Kwa habari nyingine bonyeza hapa !

Breaking News! Mwanafunzi Muhimbili Akutwa Amekufa Chumbani Kwake

Hivi Punde: Mwanafunzi wa mwaka wa tatu Shahada ya Famasia katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Edward Kahitwa amekutwa akiwa amefariki chumbani kwake, chuoni hapo. Afisa Uhusiano wa chuo hicho, Hellen Mtui amethibitisha.

RC MAKONDA APOKEA VIFAA VYENYE THAMANI MILION 400 KWAAJILI YA UJENZI WA OFISI ZA WALIMU

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amekabidhiwa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi Million 400 kutoka kiwanda cha MMI Steel ltd kwaajili ya kampeni ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu Dar es salaam. Vifaa alivyokabidhiwa ni Mabati 15,000 yenye thamani ya shilingi Million 360, Nondo Tani 22 zenye thamani ya million 40 ambapo kiwanda hicho kimemuahidi tena kumpatia RC Makonda vifaa vingine ikiwemo Rangi, Nondo na Mabati. Akipokea vifaa hivyo RC Makonda ameshukuru kiwanda cha MMI Steel chini ya mkurugenzi wake Subhash Patel kwa kuwa mdau mkubwa wa kampeni ya ujenzi wa ofisi za walimu na kuwasihi wadau na wananchi kujitokeza kuchangia kampeni hiyo ili kutoa heshima kwa walimu. Aidha RC Makonda amesema kampeni ya ujezi wa ofisi za walimu inaendelea vizuri ambapo hivi karibuni atapokea kontena nyingine 16 za furniture kutoka Marekani, Kontena 10 za Vitabu kwaajili ya Maktaba ya jamii kutoka Marekani, Kontena 10 za vifaa tiba kutoka uingereza na kontena 10 za ...

Jimbo la Mbagala Kutenganishwa-Ofisi ya Rais TAMISEMI

Serikali kupitia Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeadhimilia kuligawa Jimbo la Mbagala lililopo jijini Dar es Salaam baada ya kuwepo kwa idadi kubwa ya wakazi wanaoishi jimboni humo na kusababisha uhaba wa upatikanaji wa huduma muhimu kutoka kwa Mbunge wao. Soma habari zingine hapa

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Ustawishaji Makao Makuu Apandishwa Kizimbani

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), Paskas Muragili na mwenzake mmoja wamepandishwa kizimbani kwa kutumia madaraka vibaya. Wanatuhumiwa kutokuweka wazi maslahi yao walipotoa zabuni ya TZS 86.1m kwa Glaciaer Investment

Serikali Imekanusha Kuhusiana Kuwakandamiza Haki za Wamasai Loliondo

Wizara ya Maliasili na Utalii imekanusha taarifa ya taasisi ya Oakland ya nchini Marekani kuwa, serikali ya Tanzania inadaiwa kukandamiza haki za Wamasai wanaoishi Loliondo. Imeeleza kuwa serikali imechukua hatua stahiki kutatua mgogoro katika eneo hilo na itatoa taarifa rasmi. Soma habari zingine kwa kina bonyeza hapa

Serikali imefuta leseni za wanaohodhi maeneo ya madini

Serikali imefuta leseni zote za kuhodhi maeneo ya madini na wamiliki wake kutakiwa kuomba upya wakizingatia sheria ya madini na kanuni zake. M/kiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula amesema, maeneo yote yaliyopewa leseni yanarejeshwa serikalini bila hakikisho la kupewa tena.

TRA Mwanza Yaanza Kuwapatia Vitambulisho Wafanya biashara wadogo.

TRA Mkoa wa Mwanza imeanza kuwasajili wafanyabiashara wadogo na kuwapatia vitambulisho kwa gharama ya shilingi 10,000  kwa kila mmoja ndani ya miaka 3, lengo likiwa ni kuwatambua ili waweze kulipa kodi na kuondokana na adha ya kusumbuliwa kwenye maeneo wanayofanyia biashara. Kwa habari nyingine zaidi bonyeza hapa

Mlipuko Watokea Kisiwa cha Hawaii.

Wakazi 1,700 wakisiwa cha #Hawaii nchini Marekani, wamehamishwa kufuatia kulipuka kwa volcano kulikoambatana na tetemeko la ardhi katika mlima Kilauea. Hali ya hatari imetengazwa katika eneo hilo huku mamlaka zikiwataka wakazi hao kuchukua tahadhari kubwa. BBC

Mzigo wa mahindi wakatalia kichwani kwa mwizi

Mkazi wa Mbezi, Dar es salaam, Frank Japhet (23) amelazimika kujisalimisha kituo cha polisi Mlandizi, Kibaha, Pwani, baada ya mzigo wa mahindi unaokadiriwa kuwa na uzito wa kg 20, anaodaiwa kuuiba kung'ang'ania kichwani. Kwa maelezo ya mtuhumuwa huyo aliyoyatoa kituoni hapo, mzigo huo wa mahindi, uliofungwa kwenye kiroba aliuiba kwa mama mmoja eneo la mtaa wa Nyambwiro, Mlandizi, Kibaha, Pwani majira ya saa 7.00 usiku wa kuamkia leo. Amesema, alipoondoka na mzigo huo hadi eneo la stendi ya Mlandizi alipokuwa auache kwa mwenzake ili arudie mzigo mwingine, mzigo huo uling'ang'ania kichwani. Amesema, alijitahidi kufanya kila aliloweza ili mzigo huo utoke kichwani ikiwa ni pamoja na kulala ili akinyanyuka ubaki chini lakini aliponyanyuka, alinyanyuka nao kichwani! Baada ya kuzunguka nao kwa muda mrefu, alidai alichoka akalazimika kujisalimisha polisi ili asije akauawa na raia wenye hasira watakapobaini kuwa ni mwizi. Mpaka sasa yuko kituo cha polisi Mlandizi...

Mafuriko yaua watu 100

Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya limesema watu takribani ya 100 wamefariki kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini humo. Idadi ya watu ambao wameachwa bila makazi imekaribia robo milioni huku shirika hilo likitoa tahadhari kwamba huenda kukazuka magonjwa yanayoenezwa na maji machafu. Maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni Tana River na Garissa, ambapo Katibu Mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu Abbas Gullet, amesema, Idadi ya walioathirika inaendelea kupanda na kwamba hatua lazima zichukuliwe kwa haraka Amesema maeneo ya pwani na kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ndiyo yaliyoathiriwa zaidi ambapo kaya takriban 42,180 zimeachwa bila makao

Kigogo wa Bandari Prosper Kimaro Asomewa Mashtaka Leo

Leo April 19, 2018 Meneja wa Fedha wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Prosper Kimaro amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kosa la kujilimbikizia mali zenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.4 zisizolingana na kipato chake halali. Kimaro anadaiwa kumiliki nyumba zenye thamani ya Bilioni 1,178,370,334, zilizopo maeneo ya Temeke DSM na magari 7 yenye thamani Shilingi Milioni 307,364,678.20. Kimaro amesomewa mashtaka yake na wakili wa serikali, Vitalis Peter mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amedai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja. Wakili Vitalis amedai mshtakiwa anakabiliwa na kosa la kujilimbikizia mali zisizolingana na kipato chake ambapo anadaiwa amelitenda kosa hilo kwa miaka tofauti kati ya 2012 na 2016. Anadaiwa mali hizo amejilimbikizia maeneo ya Temeke DSM akiwa mtumishi wa umma wa TPA kama Meneja wa Fedha, amekutwa na mali zisizolingana na kipato chake halali cha zamani na cha sasa. Mali hizo ...

Diwani na Msanii Baba Levo Ampiga Daktari Kisa Vibarua

​ MSANII BABA REVO AMBAYE NI DIWANI AMPIGA DAKTARI KISA KUCHELEWA KUWALIPA VIBARUA ​ Diwani wa Kata ya Mwanga Kaskazini  Mkoani Kigoma Revokatus Kipando maarufu kwa jina la Baba Levo amemdhalilisha kwa kumpiga Dk. wa Zahanati ya  Msufini iliyoko mkoani kigoma   kwa kosa la kuchelewesha kuwalipa vibarua waliokua wanafanya ukarabati katika zahanati  hiyo. Daktari huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema diwani alifika nakuanza kumdhalilisha na kumkashifu kwa kuchelewesha kuwalipa wafanyakazi hao  mbele ya wagonjwa  na kusababisha wagojwa kuondoka pasipo kutibiwa. “Amefika  hapa kwa kufoka, kunitukana , kufanya vurugu ofisini na kanipiga, kisa pesa zilizo nje ya uwezo wangu ambazo zilikua na utaratibu za kufuatiliwa lakini hataki kufuata taratibu za kazi amehatalisha amani ya maisha yangu  na hii siyo mara ya kwanza na yuko kinyume cha sheria,” alisema Daktari huyo. Kwa mjibu wa mashuhuda wa tukio hilo akiwemo  Muugu...

Shaka ataja kila kitu walivyomtumbua Jokate

Shaka ataja Sababu za Jokate kutenguliwa katika nafasi Yake. Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ndugu  Shaka Hamdu Shaka amesema kutenguliwa kwa uteuzi wa Kaimu Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi jumuiya hiyo, Jokate Mwegelo ni maazimio yaliyoridhiwa na Baraza Kuu la Jumuiya hiyo. Uamuzi wa kutenguliwa kwa uteuzi huo wa Jokate Mwegelo, umetangazwa Leo na Mwenyekiti wa UVCCM,  Ndugu Kheri James mjini Dodoma Leo Jumapili Machi 25 2018, Kufunga Kikao cha Baraza Kuu la jumuiya hiyo, iliyotanguliwa na semina elekezi huku akisisitiza nafasi hiyo itajazwa baadaye. Akizungumza Ndugu Shaka amesema sababu za kutenguliwa kwa Jokate inatokana na uamuzi wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja huo iliyokutana kwa dharura Leo mchana chini ya Mwenyekiti wake, Ndugu  Kheri James na kuazimia kwa pamoja ambapo hatua hiyo ni utaratibu wa kawaida wa vikao vya baraza hilo ambapo ajenda inapowasilishwa bila kujali aliyewasilisha ni nani na kikao kinaporidhia inakuwa n...

Jokate Atupwa Nje na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, hana cheo tena.

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa atengua uteuzi wa Jokate. Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndugu Kheri James ametengaza kutengua uteuzi wa kaimu katibu wa idara ya uhamasishaji na chipukizi ya UVCCM Taifa Ndugu Jokate Mwegelo kuanzia Leo March 25, 2018. Pia mwenyekiti huyo amesema nafasi hiyo itajazwa baadae, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Kheri James ameyasema hayo Leo wakati wa kufunga kikao cha Baraza kuu Taifa. Jokate alikuwa anafanya kazi ya kuhamasisha vijana kuhusu maendeleo. Tutaendelea kukujuza habari hizi kila zinapotufikia.

Mwakibinga Awaamshia Dude Maaskofu wa KKKT Waliotoa Waraka 24/03/2018

WATETEZI WA RASILIMALI WASIO NA MIPAKA (WARAMI) TAARIFA KUHUSIANA NA WARAKA WA MAASKOFU KKKT ............................................................................................ JANA tuliona katika mitandao ya kijamii waraka wa viongozi wetu wa dini,ukizungumzia masuala mbali mbali ya nchi na mwelekeo wake huku sehemu kubwa ya waraka huo ukijikita katika kuikosoa serikali juu ya namna inavyoendeshwa. Tunafahamu viongozi wa dini wana wajibu wa kiutumishi katika jamii huku wakilinda dhamira yao ya kuhakikisha umoja wa nchi yetu unabaki kuwa salama kwa namna yoyote ile. Inapotokea mazingira yoyote ya viongozi wetu wa dini kushindwa kusimamia wajibu huo jamii inayoongozwa na viongozi hao inapaswa ijisimamie yenyewe na kuwakumbusha wajibu wao huo Sisi  Watetezi wa Rasiliamli wasio na mipaka (WARAMI) tunaamini kuwa moja wa wajibu wetu ni kuhakikisha  Jamii inapatiwa haki hiyo pasipo upendeleo wa aina yoyote ule wa kiimani, kisiasa kanda au hata kiuka...

Ajali Yamaliza Familia za Watu Wengi.

Watu 24 wafariki katika ajali iliyousisha Hiace na Lori. Watu 24 wamefariki na wengine 10 wamejeruhiwa kwa ajali baada ya gari aina ya hiace kugongana na lori katika kijiji cha Mparanga wilayani Mkuranga mkoani Pwani. Kaimu kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Kibiti, Mohamed Likwata amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kwamba ajali imetokea usiku wa kuamkia leo Machi 25, baada ya hiace hiyo kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa likitokea koani Mtwara kuelekea Dar es salaam. Kamanda Likwata ameendelea kwa kutaarifu kuwa majeruhi wote wamepelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili  jijini Dar es Salaam kwa matibabu.

Vyuo 163 vyapata pigo kutoka NACTE

NACTE yafungia vyuo 163 kufanya Udahili. Na Reuben Paul. Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte), imevipiga marufuku takribani vyuo 163 vilivyopo nchini Tanzania kuacha kuwafanyia udahili wa masomo wanafunzi wanaotarajia kujiunga na elimu ya juu kwa mwaka 2018 kutokana na kutokidhi vigezo. Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Udahili Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Twaha Twaha Leo (Machi 23, 2018) wakati walipokuwa wanazungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kusema baraza linawataka waombaji wa nafasi za mafunzo kwa ngazi za Astashahada na Stashahada kwa muhula wa masomo wa Machi/Aprili, 2018 kuomba kwenye vyuo vilivyokidhi ubora ambavyo vimeorodheshwa kwenye tovuti ya baraza na sio vinginevyo. "Baraza lilifanya uhakiki 'academic audit' kwenye vyuo vyote ambavyo vimesajiliwa na baraza ili kuweza kujiridhisha kuona kwamba vina sifa na mambo mbalimbali ambayo yanahusika na utoaji wa taaluma", amesema Twaha. "Katika uhakiki huo, Baraza ...

Jeshi la Korea Kaskazini, je ni imara?

Wachambuzi wa masuala ya kimataifa kupitia Televisheni ya The Fox wamechambua kuhusu silaha zilizoonyeshwa siku ile zilikuwa ni silaha kweli au zilikuwa fake, mchambuzi huyo Pregent amesema zile silaha zilikuwa fake na Kim Jong-un alifanya hivyo kwa makusudi ili askari wake wasije wakajidhuru hapo walipokuwa wakionyesha ukakamavu kwenye paredi , pia Pregent amegusia kuhusu hao wanajeshi walikuwa ni makomando au recruiter amesema hao ni makomando wote , lakini licha ya kuwa ni komando au sio komando na suala la silaha feki yasichukuliwe kama mambo ya kawaida kwani vita ni vita na sio ya siku moja maana itaacha madhara makubwa sana. Despite the fakes, a reason to fear There may be questions about North Korea’s capabilities when it comes to effectiveness on the ground, ballistic missiles and even nuclear capabilities, but experts agree that the artillery units being tested this week present a clear and presen...