Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya limesema watu takribani ya 100 wamefariki kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini humo.
Idadi ya watu ambao wameachwa bila makazi imekaribia robo milioni huku shirika hilo likitoa tahadhari kwamba huenda kukazuka magonjwa yanayoenezwa na maji machafu.
Maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni Tana River na Garissa, ambapo Katibu Mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu Abbas Gullet, amesema, Idadi ya walioathirika inaendelea kupanda na kwamba hatua lazima zichukuliwe kwa haraka
Amesema maeneo ya pwani na kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ndiyo yaliyoathiriwa zaidi ambapo kaya takriban 42,180 zimeachwa bila makao
Comments