Wiki mbili baada ya ofisi za mawakili ya Prime Attorneys jijini Dar es Salaam kuvamiwa usiku wa manane na watu wasiojulikana, ofisi nyingine ya mawakili imefanyiwa uhalifu wa aina hiyo mjini hapa. Katika uvamizi wa ofisi za mawakili za Prime Attoneys ambao pia wanamteta mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji, wezi waliiba sefu ya fedha na nyaraka baada ya kumfunga kamba mlinzi. Mmoja wa mawakili wa kampuni hiyo, Hudson Ndusyepo alisema katika uvamizi wa ofisi hizo zilizopo kwenye jengo la Prime House, Mtaa wa Tambaza, Upanga nyaraka za mfanyabiashara huyo hazikuibwa. Wakati uvamizi wa ofisi hizo ukiacha utata, watu wasiojulikana walivunja na kuiba mali mbalimbali katika ofisi mbili za mawakili jijini Arusha tukio ambalo limeibua hali ya hofu na sintofahamu kwa baadhi ya mawakili. Ofisi zilizovamiwa ni za Ideal Chambers iliyopo jengo la Blue Rock na Equality Attorneys yenye maskani yake katika jengo la Said Kondo zote zikiwa katikati ya jiji. Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Charles Mk...
Usipitwe na Habari za Kila Kona ya Dunia.