Skip to main content

Posts

Showing posts with the label Habari za Mastaa

Alikiba na Studio Mpya

Kwa mara ya kwanza mwimbaji Alikiba amezungumzia studio yake mpya baada ya kupost picha za muonekano wake. “Studio yangu mara nyingi napenda kufanya kazi na Producers tofauti, nawaalika na Producers wakubwa wanakuja tunafanya nao kazi vilevile kuna Producers tupo nao ni wachanga, nitasema lini zitaanza kufanya kazi ila bado tunafanya kazi, ni kwaajili ya King’s Music, Tutawapa updates baadae kama ni studio za video au audio tu”

Hiki ndicho chanzo cha Kifo cha Agnes Masogange

Agnes Gerald amefariki leo muda wa mchana alipokuwa akitibiwa katika hospitali ya Dokta Ngoma Jijini Dar es Salaam. Agnes alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kupungukiwa damu na ugonjwa wa mapafu.  Agnes Gerald (Masogange) ni Model na Video Queen wa muda mrefu sana Tanzania. Aliwahi kufanya ngoma na mwanamziki Belle 9 Masogange kutokea kwenye huo wimbo Belle 9 alimpatia jina hilo la Masogange. Kutokea kwenye wimbo huo Agnes Gerald alipata umaarufu mkubwa sana Tanzania kwenye Tasnia ya mziki. Learn more, then put them in mind, live it!

Jokate Atupwa Nje na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, hana cheo tena.

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa atengua uteuzi wa Jokate. Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndugu Kheri James ametengaza kutengua uteuzi wa kaimu katibu wa idara ya uhamasishaji na chipukizi ya UVCCM Taifa Ndugu Jokate Mwegelo kuanzia Leo March 25, 2018. Pia mwenyekiti huyo amesema nafasi hiyo itajazwa baadae, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Kheri James ameyasema hayo Leo wakati wa kufunga kikao cha Baraza kuu Taifa. Jokate alikuwa anafanya kazi ya kuhamasisha vijana kuhusu maendeleo. Tutaendelea kukujuza habari hizi kila zinapotufikia.

Ndala ya Diamond Platnumz yakatika mahakamani

  Habari kwa Ufupi Msanii huyo alianza kuchechemea kuonyesha mguu wake wa kushoto kulikuwa na tatizo. Ghafla alibadili mwelekeo na kwenda kwenye gari. Kilichotokea hapo ni kwamba ‘sendozi’ yake ilikuwa imekatika. Dar es Salaam, Waswahili  wanamsemo wao usemao ajali kazini. Hivyo ndivyo ilivyotokea kwa Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond ambaye amewasili katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Kisutu lakini amekutana na balaa baada ya kiatu alichovaa kukatika. Msanii huyo alianza kuchechemea kuonyesha mguu wake wa kushoto kulikuwa na tatizo. Ghafla alibadili mwelekeo na kwenda kwenye gari. Kilichotokea hapo ni kwamba ‘sendozi’ yake ilikuwa imekatika. Msanii huyo alionekana kuendelea na shughuli iliyompekeka mahakani hapo huku akiwa amekaa nje kwenye bechi pamoja na wakili wake kusubiri utaratibu. Diamond ambaye aliambatana na mwanasheria wake, akiwa katika gari aina ya Land Cruiser Prado rangi ya bluu mpauko. Mara baada ya kuwasil...