Mwenyekiti wa UVCCM Taifa atengua uteuzi wa Jokate.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndugu Kheri James ametengaza kutengua uteuzi wa kaimu katibu wa idara ya uhamasishaji na chipukizi ya UVCCM Taifa Ndugu Jokate Mwegelo kuanzia Leo March 25, 2018.
Pia mwenyekiti huyo amesema nafasi hiyo itajazwa baadae, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Kheri James ameyasema hayo Leo wakati wa kufunga kikao cha Baraza kuu Taifa.
Jokate alikuwa anafanya kazi ya kuhamasisha vijana kuhusu maendeleo. Tutaendelea kukujuza habari hizi kila zinapotufikia.
Comments