Kwa kawaida mwanamke hutokwa na majimaji mepesi (vaginal fluids) yenye rangi nyeupe au ya njano.
Inapotokea anatokwa na majimaji yenye ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali na muwasho, hiyo huwa ni ishara ya ugonjwa uitwao wa kutokwa uchafu ukeni ujulikanao kwa kitaalamu kama ‘Vaginosis’.
Mwanamke mwenye tatizo hili hujisikia vibaya na anaweza akaacha kushiriki tendo la ndoa ama kwa kuhofia maumivu au kwa kuona aibu kwani mwanaume ni vigumu kuvumilia harufu hiyo au hata kuuona tu huo ute ute kwani humjengea hisia kwamba mwenza wake atakuwa na magonjwa ya zinaa au si mwaminifu kwa ujumla.
Kinachosababisha kutokwa na uchafu ukeni:
• Kuwa na wapenzi wengi
• Baadhi ya dawa za uzazi wa mpango
• Kusafisha uke kwa kutumia dawa zenye kemikali
• Uchafu
• Uvutaji sigara
• Pombe
• Maambukizi ya Bakteria au bakteria wabaya wanapozidi ukeni
Dalili:
• Kutokwa na uchafu usio wa kawaida
• Kutokwa na uchafu wenye harufu kali kama shombo ya samaki au kitu kilichooza
• Kuwashwa sehemu za siri na ndani ya uke
• Uke unaweza kubadilika na kuwa na rangi nyekundu
• Maumivu sehemu za siri wakati wa kukojoa
• Maumivu makali chini ya kitovu
• Kutokwa uchafu uliochanganyika na damu
Matibabu
Mara uonapo dalili hizo unashauriwa kwenda kumuona daktari haraka iwezekanavyo kwa vipimo zaidi na dawa zaweza kuwa ni za kunywa au za kupaka.
Pia unaweza kutumia dawa za asili zifuatazo:
1. Kitunguu Swaumu
Kitunguu swaumu ndiyo dawa ya asili nzuri kuliko zote kwa ajili ya maambukizi ya maambukizi ya bakteria kwa wanawake. Kitunguu swaumu ni antibiotiki ya asili na hufanya kazi ya kuua bakteria wasababishao huu uchafu ukeni bila shida yoyote.
Menya punje 3 au 5 za kitunguu swaumu, zipondeponde kidogo na uzifunge vizuri ndani ya kitambaa laini na ingiza ndani ya uke wako kwa masaa 6 hivi kisha ukitoe.
Pia menye punje 6 za kitunguu swaumu na uzikate vipande vidogo vidogo (chop) na unywe na maji nusu lita asubuhi ukiamka au usiku unapoenda kulala kwa wiki mbili mpaka tatu.
2. Mtindi
Chukua mtindi ujazo wa kijiko kidogo cha chain a utumbukize ndani ya uke wako na uache huko usiku mzima. Mtindi una bakteria wazuri wanaohitajika ukeni kuweka sawa usawa wa PH (alikalini na asidi) na hivyo kuondoa maambukizi.
Pia unashauriwa kula tu huu mtindi mara mbili kwa siku kuongeza kinga ya mwili wako kwa ujumla dhidi ya magonjwa mbalimbali
3. Siki ya tufaa
Chovya pamba ndani ya siki ya tufaa (apple cider vinegar) na uweke ndani ya uke kwa dakika 15 hadi 20 kila siku na bakteria wabaya wote watakufa.
4. Uwatu
Loweka kijiko kidogo cha mbegu za uwatu (fenugreek seeds) ndani ya maji glasi moja na uache kwa usiku mzima. Kesho yake asubuhi maji haya yaliyolowekwa mbegu za uwatu kabla ya kula au kunywa chochote. Uwatu husaidia kuweka sawa homoni za mwili na kuweka sawa mzunguko wa hedhi.
5. Maziwa na binzari
Changanya kijiko kimoja cha chai cha binzari (manjano) ya unga na kikombe kimoja cha maziwa ya moto na unywe yote. Fanya hivi mara mbili kila siku mpaka tatizo litakapoisha.
6. Lemonade
Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau na asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi:
*Chukua asali mbichi nusu Lita
*Chukua limau kubwa 12 au zaidi, zikate katikati kila moja. Zikamuwe moja baada ya nyingine kupata maji maji ya limau mpaka umepata ujazo wa nusu lita.
*Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya mdalasini ya unga vijiko vikubwa 10 na maji lita 2 na nusu na uchemshe kama chai kisha ipua na uchuje na usubiri ipowe iwe ya uvuguvugu kidogo.
*Sasa changanya pamoja asali nusu lita, juisi au maji maji ya limau nusu lita, maji ya uvuguvugu ya mdalasini lita 2 na nusu ongeza na ya maji ya kawaida lita 1 kupata lita 5, chuja vizuri. Ihifadhi katika friji isiharibike.
Kunywa robo lita (ml 250) kutwa mara 2 kwa siku 10 kwa mtu mzima na glasi ndogo moja kwa siku kwa mtoto wa miaka miwili mpaka kumi.
Unaweza pia kuongeza majani kidogo ya mnanaa (mint) na mbegu za shamari (fennel seeds) ili kuongezea radha na harufu nzuri. Kunywa juisi hii kila unapokuwa umepata chakula cha mchana cha nguvu au cha jioni.
7. Jeli ya mshubiri (aloe vera jel)
Ingawa jeli fresh ya mshubiri haitibu moja kwa moja tatizo la kutokwa na uchafu ukeni inaweza kuwa msaada mkubwa katika kupunguza maumivu na muwasho ukeni.
Chana kipande kidogo cha jani la mmea huu na ukamue kidogo kupata maji maji yake na upake vizuri taratibu ndani ya uke mara mbili kwa siku kwa majuma kadhaa hadi muwasho utakapoisha.
8. Bamia
Bamia husaidia kuondoa maji maji na makohozi kwenye mfumo wako wa mwili.
*Chukua bamia gramu 100
*Zikatekate vipande vidogo vidogo
*Weka kwenye sufuria ongeza maji nusu lita na uchemshe mpaka maji yamebaki robo ndani ya sufuria
*Ipua na uchuje
*Gawanya hayo maji uliyochuja katika sehemu mbili na unywe sehemu moja asubuhi na nyingine jioni kila siku mpaka umepona
9. Komamanga
Komamanga ina sifa ya kuwa dawa na inaweza kutumika kama dawa ya kutibu uchafu ukeni. Vyote majani yake au mbegu zake vinaweza kutumika kwa ajili hii.
Kunywa glasi moja ya juisi ya komamanga kutwa mara moja kwa mwezi mmoja hivi mpaka umepona.
MAMBO MHIMU YA KUZINGATIA:
Zingatia dawa peke yake hazitofaa kitu bila kuzingatia ushauri au masharti mhimu yafuatayo:
1. Kunywa maji mengi kila siku kuanzia glasi 8 hadi 10
2. Tumia zaidi vyenye vitamini B, C, D na E
3. Tumia sana matunda hasa machungwa, limau, ndizi na vitunguu
4. Punguza vyakula vyenye wanga
5. Acha kutumia vidonge vya uzazi wa mpango, hii ni kwa sababu vidonge hivi vinasemwa huwa vinasababisha kushuka kwa kinga ya mwili na kukufanya mrahisi kupata maambukizi ya fangasi.
6. Epuka mapenzi kinyume na maumbile
7. Acha kutumia sukari na badala yake tumia asali
8. Usitumie chokoleti na vitu vingine vya namna hiyo
9. Kuwa na mpenzi mmoja tu
10. Pendelea kujiweka msafi muda wote
11. Oga maji ya moto
12. Acha vinywaji baridi, acha pia chai ya rangi na kahawa
13. Acha vilevi
14. Acha matumizi ya pafyumu hasa maeneo ya huko
Mhimu: Kama una swali au unahitaji ushauri zaidi comment hapo chini nitakujibu.
Je umewahi kuugua ugonjwa huu na ukapona? kama ndiyo ulitumia dawa gani? nitashukuru ukiniambia dawa uliyotumia mpaka ukapona ili nisaidie na wenzako wengine.
Share na wenzio kwenye magroup ya facebook na watsup http://paulreuben59.blogspot.com
Comments