Skip to main content

Posts

Showing posts from January, 2020

Marekani iko 'tayari kufanya mazungumzo' na Iran

aza habari hii Facebook   ambaza habari hii Messenger   Sambaza habari hii Twitter   Sambaza habari hii Email   Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha EPA Marekani imesema iko "tayari kujadiliana na Iran bila masharti" baada uhasama uliozuka baina ya nchi hizo kufuatia mauaji ya jenerali Qasim Soleimani. Katika waraka wake kwa Umoja wa Mataifa, Marekani ilijitetea kuwa ilimuua jenerali wa jeshi la Iran Qasem Soleimani kama hatua ya kujilinda.  Iran ilijibu hatua hiyo kwa kushambulia kwa makombora kambi ya majeshi ya Marekani nchini Iraq japo hakuna mtu aliyejeruhiwa. Jenerali Soleimani ilichukuliwa kuwa afisa wa pili wa ngazi ya juu nchini Iran. Iran yashambulia kwa makombora kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq Gharama za mafuta zapanda baada ya mashambulizi Iraq Kama mkuu wa kikosi maalum cha Quds Force, katika jeshi la ulinzi la Revolutionary Guards' alilikuwa mtekelezaji wasera za Iran katika eneo la mashariki ya kati. Kiongozi

Ndege ya Ukraine yaanguka Iran ikiwa na abiria 180, Abiria wote wafariki

Ndege ya Ukraine aina ya Boeing-737 iliyokuwa na abiria 180 imeanguka Iran, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo. Watoa huduma wa msalaba mwekundu wa Iran wanasema kuwa hakuna dalili yeyote kama kuna mtu aliyepona katika ajali hiyo. Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la kimataifa la ndege la Ukraine ilianguka muda mfupi baada ya kuanza safari katika uwanja wa ndege wa Imam Khomeini mjini Tehran. Ripoti za awali zinadai kuwa ndege hiyo ilikuwa safarini kuelekea mji mkuu wa Ukraine, Kyiv.  Haijabainika ikiwa ajali hiyo ina uhusiano wowote na mzozo wa Iran-na Marekani. Kikosi cha uokoaji tayari kimetumwa katika eneo la tukio karibu na uwanja wa ndege, eneo ambalo ndege lilianguka. Credit: GettyImage " Ndege imeshika moto na tumetuma kikosi huko ... ," kiongozi wa huduma za dharura Pirhossein Koulivand,ameviambia vyombo vya habari ambapo Reuters imeripoti. Je tutegemee machafuko zaidi kutokea? Endelea kuwa pamoja nasi bega kwa bega, mshirikishe na mwenz