Habari kwa Ufupi
Msanii huyo alianza kuchechemea kuonyesha mguu wake wa kushoto kulikuwa na tatizo. Ghafla alibadili mwelekeo na kwenda kwenye gari. Kilichotokea hapo ni kwamba ‘sendozi’ yake ilikuwa imekatika.
Dar es Salaam, Waswahili wanamsemo wao usemao ajali kazini. Hivyo ndivyo ilivyotokea kwa Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond ambaye amewasili katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Kisutu lakini amekutana na balaa baada ya kiatu alichovaa kukatika.
Msanii huyo alianza kuchechemea kuonyesha mguu wake wa kushoto kulikuwa na tatizo. Ghafla alibadili mwelekeo na kwenda kwenye gari. Kilichotokea hapo ni kwamba ‘sendozi’ yake ilikuwa imekatika.
Msanii huyo alionekana kuendelea na shughuli iliyompekeka mahakani hapo huku akiwa amekaa nje kwenye bechi pamoja na wakili wake kusubiri utaratibu.
Diamond ambaye aliambatana na mwanasheria wake, akiwa katika gari aina ya Land Cruiser Prado rangi ya bluu mpauko.
Mara baada ya kuwasili katika viunga vya Mahakama ya Kisutu alipitiliza moja kwa moja hadi Mahakama ya Watoto iliyopo ndani ya viunga vya Mahakama ya Kisutu.
Comments