Pengine ulikuwa hujawahi kusikia au kufahamu kama unaweza kupunguza uzito bila hata kutumia madawa ya Hospitali. Zifuatazo ni dondoo kuhusiana na kupunguza uzito.
1.Juisi ya mchanganyiko wa ndizi na mizabibu.
Kifungua kinywa hiki kilaini kinawafaa wote akina mama na akina baba ambao wana tatizo la uzito uliopita kiasi, kinywaji hiki kitakusaidia kupunguza uzito kwa mda mfupi. Juisi hii ni rahisi kuiandaa nyumbani mda wa asubuhi maana haihiyaji gharama kubwa ya uandaaji.
Kifungua kinywa hiki kina virutubisho vya afya kama vile nyuzinyuzi(fiber), Vitamin A&C, Kabohaidreti, Kalsiamu, Sodiamu, Protini na madini ya Chuma.
2. Mchanganyiko laini wa juisi ya komamanga(pomegranate) na tunda nyanya(strawberry).
Tunda nyanya na komamanga yote ni matunda ya msimu hivyo mda wake ukifika inatakiwa tuyatumie sana mda wa asubuhi kwa kutengeneza juisi ya matunda haya kwa ajili ya kupunguza uzito. Matunda yote haya yana viini lishe ambavyo vina uwezo wa kukinga seli za mwili zisiharibiwe na chembechembe haribifu(free radical) ambazo huweza kusababisha saratani.
Kinywaji hiki kinaandaliwa kwa mchanganyiko wa Spinachi, Tunda nyanya(strawberry), Komamanga(pomegranate) na maji ya nazi.
3.Juisi ya kijani
Kinywaji kilaini cha kijani ni mchanganyiko wa mboga za majani na matunda ambayo husaidia kuongeza nguvu na kinga ya mwili. Kwa watu wote ambao wana matatizo ya uzito mkubwa na wana hitaji kupunguza uzito chaguo ni lako sasa kuandaa juisi hii asubuhi kila siku.
Kinywaji hiki kina madini na vitamini muhimu sana kwa ajili ya kupunguza uzito wa mwili wako.
4.Green Monster
Huu ni mchanganyiko wa ndizi, spinach, Almond maziwa, cream na mbegu chia(chia seeds), hii nin juisi nyingine tena ambayo itakusaidia kupunguza uzito kwa haraka zaidi. Pamoja na kuwa na mchanganyiko wote huo wa matunda juisi hii ina radha tulivu ya kuvutia na itakayomfanya mtumiaji aipende juisi hii.
Juisi hii ina virutubisho kama vile Sodiamu, nyuzinyuzi na protini.
5. Bluuberi na komamanga
Tengeneza juisi yako ya bluuberi na komamanga kwa mchanganyiko ufuatao kale, bluuberi, komamanga na mbegu chia baada ya kuchanganya utaipata rangi ya zambarau kwenye juisi yako. Juisi hii itakuwa na radha ya beri na komamanga.
Kwa watu ambao wanahitaji kupunguza uzito ni lazima watumie juisi hiikama kifungua kinywa kabla hawajatumia chakula chochote. hii inasaidia kuyachoma mafuta(fats) kwa haraka zaidi na mtumiaji atayaona mabadiliko kwa mda wa mwezi mmoja tu. Madini na virutubisho vinavyopatikana kwenye juisi hii ni kabohaidreti, protini, sodiamu, nyuzinyuzi, kalsiumu, vitamini A&C na madini ya chuma.
6. Juisi ya ndizi, bluuberi na chai ya kijani
Huu ni mchanganyiko mwingine tena wa kifungua kinywa chenye kirutubisho laini ambacho mkinasaidia kupunguza uzito wa mwili wako. Mtu anaweza kutumia mchanganyiko huu kila siku asubuhi na tajisikia vizuri tu baada ya mda mfupi. Chai ya kijan i ni moja ya kinywaji kizuri kwa kupunguza unene kwa sababu ina viini vinavyolinda seli za mwili zisiharibiwe(Antioxidanti). Ni rahisi sana kuandaa mchanyiko huu kwa ajili ya kifungua kinywa.
7.Mchanganyiko wa matunda ya Cran-peach.
Huu ni mchanganyiko mwingine unaopunguza uzito ambapo husaidia kutoa mafuta yote ya ziada yaliyopo ndani ya mwili wako kwa kuyavunjavunja na baadae kuyatoa nje ya mwili kwa kupitia viungo vya mwili wako yaweza kuwa ngozi, mkojo au haja kubwa. Kinywaji hiki kina mchanganyiko wa matango, peach, yorgut na juisi ya cran-beri. Virutubisho vilivyomo ni sodiamu,protini, nyuzinyuzi na kabohaidreti.
8.Mchanganyiko wa Almondi maziwa, peanut butter, na strawberry.
Mchanganyiko huu sio tu kuwa una radha nzuri lakini pia unaweza kubadilisha maisha yako kwa kupunguza uzito wa mwili wako. Juisi hii ina virutubisho vya afya kama vile sodiamu, protini na nyuzinyuzi; Mchanganyiko huu pia huitwa PB&J Protini ambao unakuwa na calorie 250-300.
9. Juisi ya Strawberi, almondi, yorgut(Greek yogurt),broccoli, Maharage ya Garbanzo,chakula cha flax na chai ya kijani.
Utumiaji wa juisi hii kama kifungua kinywa kitakusaidia katika mfumo mzima wa umeng'enyaji wa chakula na kukuletea hamu kula. Ni rahisi sana kuutengeneza mchanganyiko huu kama matunda yaliyotajwa hapo juu. Virutubisho vinavyopatikana kwenye juisi hii ni sodiamu,potassiamu, nyuzinyuzi, protini, vitamini A&C, chuma na kalisiamu.
Je, leo utatumia juisi ipi kati ya hizo?
Ili uwe wa kwanza kupata masomo haya kila siku Usiache ku-subcribe kwenye blog hii.
Tutumie maoni yako.
Comments