Kuna mahusiano makubwa sana kati ya miili yetu na ubongo au mfumo wa fahamu. Jinsi mwili ulivyo na unavyofanya kazi ni kwa sababu tu ya ishara za ubongo wetu kufanya kazi. Na ili ubongo ufanye kazi yake vizuri ni lazima tuwe na afya bora, maisha ya afya sio tu kwa afya ya mwonekano bali pia katika afya ya ubongo. Na hii inawezekana kwa kuwa mbali na vitu au vyanzo vya sumu na miale mbalimbali lakini pia na uchafu ambao huifanya miili ichoke tu pasipo sababu na kujisikia kukerwa sana.
Kuna vyakula vingi vya kuleta afya na vyakula hivyo vipo katika mazingira yetu tunayoishi, vyakula hivyo hufanya kazi ya kupunguza sumu na kumaliza kabisa sumu mwilini.
- Tangawizi (Ginger)
- Tangawizi inatumika hasa kwenye chakula na dawa tangu miongo mingi iliyopita na bado inaaminiwa ni moja ya kiuongo chenye faida au mzizi bora wenye faida kwenye mwili wa biladamu.
- Tangawizi hutumika kutoa sumu mwilini kutokana na maji machafu uliyokunywa au chakula kichafu na husafisha mpaka kwenye Ini.Hutumika kwenye vyakula, dawa na vinywaji.
- Chai ya tangawizi hutumiwa sana na watu wa aina zote, na hutibu kwa mtu aliye na madonga ya koo(sore throat itching).
- Tangawizi unaweza ukaisaga na kuweka unga wake kwenye maji ya kunywa nayo ni njia bora ya kuitumia tangawizi kwa ajili ya kutoa sumu mwilini.
2.Kitunguu saumu (Garlic)
- Husaidia kwenye Ini na kuongeza kinga ya mwili. Ini hufanyiwa usafi na kitunguu hiki na baadae Ini hufanya kazi kwa ufanisi zaidi siku hadi siku
- Kitunguu hiki huongeza nguvu mwilini na katika mfumo wa kupambana na bacteria na virusi mbalimbali ambavyo havijakuwa sugu.
- Lakini pia ni kiungp kinachoongeza radha kwenye chakula na unapokula unajisikia kuwa umekula mlo ulio mzuri sana.
3.Broccoli (Brokoli)
- Kwa kuwa hii ni mboga huwa ni ya kijani , ina madini mengi sana ya muhimu na vitamini lakini pia ina virutubisho vingi na vya kukinga miili yetu.
- Brokoli hugeuza sumu mbalimbali ndani ya mwili na hiyo sumu inarudishwa kuwa virutubisho tena na kuliacha ini likiwa safi.
- Brokoli unaweza kukata na kula jinsi ilivyo lakini pia inakuwa tamu zaidi inapopikwa kwenye moto mdogo.
4.Cabbage
- Ni mboga ambayo inahitajika sana kwa sababu ina kiwango kidogo cha calories na pia hupunguza kiwango cha mafuta mwilini.
- Cabbage ina nyuzinyuzi na ndio maana ukila cabbage lazima utakwenda tu chooni kwa sababu inasaidia kupata choo, lakini pia kutokana na majimaji yake hufanya kupata haja ndogo mara nyingi na hivyo hutoa uchafu mwingi mwilini.
5. Beetroot (Magimbi)
- Beetroot ina virutubisho vingi ambavyo husaidia kupambana na vimelea na pia inazuia kansa, kumbe hufanya kazi kama kinga ya Kansa.
- Beetroot inasaidia kusafisha sumu yote na kuhakikisha hata sumu yote imetoka na isirudi tena, maana kuna sumu ambazo zina tabia ya kutoka na kurudi tena polepole ndani ya mwili.
- Kama unapenda kutoa sumu mwilini tumia hii njia itakusaidia.
Limeandaliwa nami Reuben kutoka
http://paulreuben59.blogspot.com
Pongezi kwa Dr.Lauren Muwezeshaji wa somo hili.
Tafadhari usikose mwendelezo wa somo hili zuri lakini pia unaweza kutuma maoni yako tutakujibu moja kwa moja.
Comments