Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amemtumia onyo kali rais wa Korea Kaskazini na kumuonya vikali Rais Donald Trump.
Rais Duterte ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za Kusini Mashariki mwa Bara la Asia (Association of Southern East Asian Nations- ASEAN) alimpigia simu Rais Donald Trump mapema siku ya jumamosi jana jioni.
Alisikika kwa uoga wake wa uwezekqno mkubwa wa kuweza kutokea vita ya nyuklia na hasa nchi yake ikiwa karibu sana na hizo nchi mbili zenye mzozo.
Rais Duterte alisema kwa namna hiyo basi watakuwa wahanga wakubwa kama vita hiyo itatokea, aliongeza na kusema kuwa na vita ni lqzima mmojq wao atakosea na kuweza kuishambulia mpaka nchi yake na kwa namna yoyote ile wanaweza kuleta majanga makubwa hasa Catastrophe.
Rais Duterte alisema ni bora vita hiyo isitokee na hata kama ikitokea alimwambia Donald Trump asiichezee mikononi mwake au nchini mwake Trump.Maana Kim Jong-un anaonekana mwenye furaha sana maana anataka kuuangamiza ulimwengu.
Maneno haya ya Duterte yalikuja baada ya jaribio la kurusha bomu lao jana kushindwa.
Lakini pia katika taarifa nyingine leo Rais Trump amenukuliwa akisema anajua huu mgogoro hautaweza kutatuliwa kwa njia ya kidiplomasia sasa hatavumilia watakapofanya jaribio lingine la bomu, na anajua hilo bomu la jana halikuwa la nyuklia ila atakaporusha bomu la Nyuklia kama jaribio hatavumilia tena.
Usikose kujiunga nami kwa taarifa zingine za habari kutoka hapahapa @ReubenHabariTz
Comments