Skip to main content

JE WALIJUA TATIZO LA FIBROIDS KWA AKINA MAMA?

TATIZO LA UVIMBE KWENYE UZAZI(FIBROIDS)NI HATARI KWA AKINA MAMA
Uvimbe Kwenye Uzazi Mahiri Kama Fibroids.
Inasemekana Kati ya 20% hadi 50% ya wanawake walio katika umri wa kuzaa,miaka 30 hadi 50,wana Fibroids.
Fibroids ni nivimbe ambazo hujishikiza katika kuta za mfuko wa Uzazi,ndani na nje ya mfuko wa uzazi au kwenye Ovari,Vimbe hizo hukuwa na kuwa na ukubwa tofauti tofauti,unaweza kuwa mdogo kama haragwe au kufikia ukubwa wa tikiti maji.
Chanzo Cha Fibroids
Sababu hasa za kuota kwa fibroids katika viungo vya uzazi vya mwanamke bado hazieleweki vizuri na inaaminika kwamba kila uvimbe wa fibroid unatokana na seli ya msuli wa uterus ambayo huwa na tabia ya tofauti na seli nyingine na hivo hukuwa kwa haraka haraka ikichangiwa na uwepo wa homoni ya estrogen.
Wanawake wanaokaribia kufikia ukomo wa kupata siku zao za mwezi wanaonekana kuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata fibroids kwa sababu ya kuwa wameishi na homoni ya estrogen kwa muda mrefu zaidi.
Wanawake wenye asili ya mchanganyiko wa wamarekani na waafrika (wamarekani weusi) nao wanaonekana kupatwa na fibroids zaidi ya wanawake wengine ingawa sababu bado haijajulikana.
Tafiti zinaonesha kuwa idadi ya wanawake wanaopatwa na fibroids katika kundi la wanawake ambao wamezaa watoto angalau wawili wakiwa hai huwa ni nusu ukilinganisha na wale ambao hawajazaa hata mara moja.
Hapa haieleweki kama kuzaa kulizuia wanawake hawa wasipate fibroids au fibroids ndizo zilizo wazuia wanawake wa kundi la pili wasizae,utafiti kuhusu hilli bado unaendelea.
Dalili Za Fibroids
Akina mama wengine wenye uvimbe wa fibroids huwa hawaoni dalili zozote zile (wengi hawajui kama wana fibroids) au kuona dalili kidogo na kwa wengine dalili hizi hujitokeza sana na kuwasumbua hadi kufikia kutafuta tiba.
Hizi ni Baadhi ya dalili za fibroids;
– Kutokwa na damu kwa wingi wakati wa siku za hedhi au kutokwa na damu kwa muda mrefu zisizo koma
– Kutokwa na damu kusiko kwa kawaida katikati ya siku za mwezi
– Mauvimu ya nyonga (uvimbe kugandamiza kwenye viungo vya nyonga)
– Kupata haja ndogo mara kwa mara
– Maumivu ya mgongo
– Maumivu wakati wa tendo la ndoa ama kukosa hamu ya kufanya tendo hilo.
– Upungufu wa damu kwa sababu ya kutokwa na damu kwa wingi wakati wa siku za hedhi.
– Maumivu ya kichwa
– Maumivu kwenye miguu
– Kuvimba sehemu ya chini ya tumbo (Fibroids kubwa)
– Uzazi wa shida
– Mimba za shida
– Kutopata mimba
– Kutoka kwa mimba mara kwa mara.
Aina Za Fibroids-Kuna aina nne za Fibroids:
1-Intramural: Fibroids aina hii hukua kwenye kuta za uterus,hii ndiyo aina ya fibroids inayowapata wanawake wengi.
2-Subserosal fibroids:
Fibroids aina hii hukua nje ya kuta za uterus na huweza kuwa na shina.Subserosal fibroids huweza kukua na kuwa kubwa sana.
3-Submucosal fibroids:
Fibrioids aina hii huota na kukua kwenye
misuli chini ya ngozi laini ya kuta za uterus.
4-Cervical fibroids:
Fibroids aina hii hujenga kwenye shingo ya tumbo la uzazi (Cervix).
Tiba Ya Fibroids
Kama mwanamke hapati usumbufu wa namna yo yote katika shughuli zake za kawaida, anaweza asipewe tiba ya aina yo yote hata kama imegundulika kuwa ana uvimbe wa fibroid kwa sababu mwanamke anapokaribia kukoma hedhi fibroids hunyauka zenyewe na mara nyingine kutoweka kabisa.
Endapo tiba ni lazima kwake,anaweza kupewa dawa au kufanyiwa upasuaji kutokana na hali iliyopo.
Tiba Ya Fibroids Kwa Kutumia Dawa,tiba kubwa ya fibroids ni kwa kutumia dawa aina ya GnRHA (gonadotropin released hormone agonist) ambayo hutolewa kama sindano.
Dawa hii huufanya mwili wa mwanamke upunguze utengenezaji wa estrogen hivyo kusababisha fibroids kunyauka.
Tiba nyingine ni Tranexamic acid, vidonge vya kuzuia maumivu, vidonge vya kuzuia mimba (kuzuia mwanamke asipate siku) na LNG-IUS (Levonorgestrel intrauterine system) ambacho ni kifaaa cha plastiki kinachowekwa kwenye uterus.
Tiba Ya Fibroids Kwa Upasuaji
Kama dawa zimeshindwa kufanya kazi, mgonjwa hufanyiwa upasuaji kwa moja ya njia zifuatazo:
Hysterectomy– Kuondoa uterus,hii hufanywa pale fibroids zinapokuwa kubwa sana au pale ambapo mgonjwa anatokwa na damu nyingi sana.
Upasuaji huu una madhara ya aina mbili:
1-Kupunguza hamu ya kufanya mapenzi
2-Kukoma hedhi mapema
Myomectomy– Fibroids kuondolewa kutoka wenye ukuta wa uterus,hii hufanyika pale ambapo mgonjwa anapenda kuendelea kuzaa.
Tiba hii haifanywi kwa fibroids kubwa au zile ambazo kwenye maeneo nyeti ya uterus.
Endometrial ablation:
Kuondolewa ngozi laini ya ndani ya uterus.
UAE (Uterine Artery Embolization):hii ni kuzuia fibroids zisipate damu na hivyo kunyauka,UAE hufanywa kwa fibroids kubwa.
Magnetic-resonance-guided percutaneous laser ablation: Sindano nyembamba hupenyezwa kupitia ngozi hadi kulifikia fibroid. Fibroid humulikwa na mionzi ya laser kupitia waya fiber-optic uliopitishwa kwenye sindano na kulinyausha Fibroid.
Magnetic-resonance-guided focused ultrasound surgery:
Kifaa maalumu hutumika kugundua eneo la fibroid, kisha mawimbi ya sauti huelekezwa kwenye fibroid. Mawimbi hayo hulinyausha fibroid.
Katika mada ya leo tumeona fibroids ni nini,chanzo cha fibroids,dalili zake,aina za fibroids na tiba zinazotumika kuondoa fibroids.
Makusudio yetu ni kwamba uelewe vyema mada hii,lakini endapo utapenda kujua namna ya kuondoa fibroids bila kutumia dawa za Medications wala kufanyiwa operation
Tunazo Food Supplements(Virutubisho) Ambavyo ni Suluhisho la Kudumu la Tatizo la Fibroids
Kwa Ushauri au Kupata Huduma zetu Popote Ulipo(Tanzania Na Zaidi Ya Nchi 160 Duniani).
Wasiliana nasi Independent Health Consultants.....
Kwa WhatsApp +255 765 273125 Or Direct Call     +255 673 273125
#Smiletoday
#Manasemasinza

Comments

Popular posts from this blog

The court system during colonialism in Tanzania.

Introduction. Pre-colonial Period Administration of justice during this time depended heavily on the social economic and political organization of the society in Tanganyika. Two systems of administration of justice namely; The Centralized and the Non-Centralized systems could be identified at the time. The Centralized Systems was applicable to societies with chiefs who played both roles of adjudicators and that of governors. In the Non-Centralized systems the entire community took part in the adjudication of disputes. However in both systems there were no formalization of procedure in adjudication, the customs of the respective societies prevailed in the process. Colonial Period The German Colonial Period. The Land currently covering Tanzania Main Land, was then included in what was called the German East Africa, it was subjected to the German Colonial Rule from 1886 up to the end of the First Ward War, 1918. During this Germany Colonial Rule the Administration of Justi...

Ndege ya Ukraine yaanguka Iran ikiwa na abiria 180, Abiria wote wafariki

Ndege ya Ukraine aina ya Boeing-737 iliyokuwa na abiria 180 imeanguka Iran, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo. Watoa huduma wa msalaba mwekundu wa Iran wanasema kuwa hakuna dalili yeyote kama kuna mtu aliyepona katika ajali hiyo. Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la kimataifa la ndege la Ukraine ilianguka muda mfupi baada ya kuanza safari katika uwanja wa ndege wa Imam Khomeini mjini Tehran. Ripoti za awali zinadai kuwa ndege hiyo ilikuwa safarini kuelekea mji mkuu wa Ukraine, Kyiv.  Haijabainika ikiwa ajali hiyo ina uhusiano wowote na mzozo wa Iran-na Marekani. Kikosi cha uokoaji tayari kimetumwa katika eneo la tukio karibu na uwanja wa ndege, eneo ambalo ndege lilianguka. Credit: GettyImage " Ndege imeshika moto na tumetuma kikosi huko ... ," kiongozi wa huduma za dharura Pirhossein Koulivand,ameviambia vyombo vya habari ambapo Reuters imeripoti. Je tutegemee machafuko zaidi kutokea? Endelea kuwa pamoja nasi bega kwa bega, mshirikishe na mwenz...