*DALILI 10 KUWA WEWE NI MVIVU*
*1. Uko busy sana lakini "For Nothing"*
Ikifika jioni unajikuta umechoka sana. Lakini ukijitafakari tangu asubuhi huna cha maana ulichokifanya. Na tangu asubuhi ulikua " bize" sana.
Huenda ulishinda Whatsapp, Facebook, Instagram, etc una"post" na ku"like" tu.
*2 Una kazi nyingi sana Jumapili*
Wakati Jumapili ikiwa ni siku ya mapumziko kwa watu wengi ili waianze wiki inayofuata wakiwa fresh, kwa mtu mvivu ni tofauti. Atakuta mrundikano wa kazi zote zinatakiwa kufanyika Jumapili.
*3 Kuna kitu kinakuambia kuwa unajirudisha nyuma mwenyewe*
Kama unahisi kila muda unajilaumu, kuwa why hukufanya hiki, why hukufanya kile, ni nini kimetokea? Imekuaje? Na kuanza kujilaumu mwenyewe kwa uzembe huo, basi jua kuwa wewe ni *Mvivu*.
*4 Una sababu zaidi ya 76 za kutofanya mazoezi*
Unajua kuwa mazoezi ni muhimu kwa ajili ya afya yako, lakini wewe mwenyewe unajipa "vijisababu" vingi sana vya kuacha mazoezi. Hii ni dalili ya *Uvivu*.
*5 Unajiuliza sana Kwanini niko hivi?*
Kwanini nashindwa kufua hadi nguo zinajaa? Kwanini sikufanya hivi jana? Kwanini ile taa kila siku nasahau kuizima? Kwanini pale ukumbini sifagii? Kwanini? Kwanini? Kwanini??.
Maswali haya yapo kichwani mwa mtu *mvivu*.
*6. Inakuchukua muda mrefu sana kujaribu kufanya kitu*.
Hata pale unapoamua kuwa "nitafanya" basi inakuchukua muda mrefu sana kuanza. Ukipewa fursa huamui kufanya hapohapo, unaacha na kujaribu "kujipa muda zaidi". Mtu mvivu hupenda shortcut, kwahiyo akiona kuna kitu kitamshughulisha huwa anaachana nacho kwa kisingizio cha "kujipa muda" au "kutafakari".
*7 Huogi, wala hupigi mswaki usiku*
Unajua umuhimu wa hivi vitu kabla ya kulala. Lakini hufanyi!!. Huna sababu ya msingi unayoweza kuieleza. Huu unaitwa *uvivu*.
*8 Huwezi kuwasaidia wengine*
Yaani hebu jiangalie mara ngapi wewe unataka kufanyiwa mambo na watu hata kama unayaweza. Upo hapo sebuleni unaangalia tv, lakini unamtaka mtu akuletee maji ya kunywa. Lakini yeye atataka umsaidie kuhusu kitu fulani, unamsubirisha .. Na hufanyi kabisa. Hii ni dalili kuu ya *uvivu*.
Mvivu hasaidii wengine.
*9 Unaangalia sana TV,hata vipindi usivyovipenda*
Ili mradi uwepo hapo kwenye sofa na kukodoa, hutaki kunyanyuka. Hata kama kipindi hukipendi lakini unakodoa kuangalia. Huwezi hata kutumia muda wako kuwasalimu wengine hata kwa sms. Huu ni uvivu.
*10. Unaweka vitu vyako bila mpangilio*
Sometimes inakupa tabu sana kutafuta kitu ulichoweka mwenyewe.. Na pengine usikione!! Kila kitu kiko vurugu. Angalia hapo kwenye sofa, hakuna shati lako? Kwanini iwe hivyo. Hii ni dalili ya uvivu.
*UVIVU* wako ni sumu ya maendeleo yako. Huwezi kuwa mtu mwenye mafanikio kama umekalia uvivu. Jitoe huko.
Comments