Skip to main content

Vyuo 163 vyapata pigo kutoka NACTE

NACTE yafungia vyuo 163 kufanya Udahili.

Na Reuben Paul.

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte), imevipiga marufuku takribani vyuo 163 vilivyopo nchini Tanzania kuacha kuwafanyia udahili wa masomo wanafunzi wanaotarajia kujiunga na elimu ya juu kwa mwaka 2018 kutokana na kutokidhi vigezo.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Udahili Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Twaha Twaha Leo (Machi 23, 2018) wakati walipokuwa wanazungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kusema baraza linawataka waombaji wa nafasi za mafunzo kwa ngazi za Astashahada na Stashahada kwa muhula wa masomo wa Machi/Aprili, 2018 kuomba kwenye vyuo vilivyokidhi ubora ambavyo vimeorodheshwa kwenye tovuti ya baraza na sio vinginevyo.

"Baraza lilifanya uhakiki 'academic audit' kwenye vyuo vyote ambavyo vimesajiliwa na baraza ili kuweza kujiridhisha kuona kwamba vina sifa na mambo mbalimbali ambayo yanahusika na utoaji wa taaluma", amesema Twaha.

"Katika uhakiki huo, Baraza lilibaini kuwa baadhi ya vyuo vilikidhi viwango vya ubora kwa mujibu wa taratibu za Baraza.  Hata hivyo, baadhi ya vyuo vilibainika kuwa na changamoto mbalimbali zinazoweza kuathiri ubora wa elimu na mafunzo yanayotolewa", amesema Twaha.

Pamoja na hayo, Twaha ameendelea kwa kusema "kufuatia zoezi hilo vyuo vyote vilivyobainika kuwa na mapungufu vilitaarifiwa na kutakiwa kurekebisha mapungufu yaliyobainishwa kabla ya kuendelea na udahili wa wanafunzi kwa mwaka mpya wa masomo 2018/2019".

Kwa upande mwingine, Twaha amesema kuwa udahili wa muhula wa Machi/Aprili, 2018 hauhusishi programu zote za kada ya Afya na Ualimu.

Comments

Popular posts from this blog

The court system during colonialism in Tanzania.

Introduction. Pre-colonial Period Administration of justice during this time depended heavily on the social economic and political organization of the society in Tanganyika. Two systems of administration of justice namely; The Centralized and the Non-Centralized systems could be identified at the time. The Centralized Systems was applicable to societies with chiefs who played both roles of adjudicators and that of governors. In the Non-Centralized systems the entire community took part in the adjudication of disputes. However in both systems there were no formalization of procedure in adjudication, the customs of the respective societies prevailed in the process. Colonial Period The German Colonial Period. The Land currently covering Tanzania Main Land, was then included in what was called the German East Africa, it was subjected to the German Colonial Rule from 1886 up to the end of the First Ward War, 1918. During this Germany Colonial Rule the Administration of Justi...

Ndege ya Ukraine yaanguka Iran ikiwa na abiria 180, Abiria wote wafariki

Ndege ya Ukraine aina ya Boeing-737 iliyokuwa na abiria 180 imeanguka Iran, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo. Watoa huduma wa msalaba mwekundu wa Iran wanasema kuwa hakuna dalili yeyote kama kuna mtu aliyepona katika ajali hiyo. Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la kimataifa la ndege la Ukraine ilianguka muda mfupi baada ya kuanza safari katika uwanja wa ndege wa Imam Khomeini mjini Tehran. Ripoti za awali zinadai kuwa ndege hiyo ilikuwa safarini kuelekea mji mkuu wa Ukraine, Kyiv.  Haijabainika ikiwa ajali hiyo ina uhusiano wowote na mzozo wa Iran-na Marekani. Kikosi cha uokoaji tayari kimetumwa katika eneo la tukio karibu na uwanja wa ndege, eneo ambalo ndege lilianguka. Credit: GettyImage " Ndege imeshika moto na tumetuma kikosi huko ... ," kiongozi wa huduma za dharura Pirhossein Koulivand,ameviambia vyombo vya habari ambapo Reuters imeripoti. Je tutegemee machafuko zaidi kutokea? Endelea kuwa pamoja nasi bega kwa bega, mshirikishe na mwenz...