Watu 24 wafariki katika ajali iliyousisha Hiace na Lori.
Watu 24 wamefariki na wengine 10 wamejeruhiwa kwa ajali baada ya gari aina ya hiace kugongana na lori katika kijiji cha Mparanga wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Kaimu kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Kibiti, Mohamed Likwata amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kwamba ajali imetokea usiku wa kuamkia leo Machi 25, baada ya hiace hiyo kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa likitokea koani Mtwara kuelekea Dar es salaam.
Kamanda Likwata ameendelea kwa kutaarifu kuwa majeruhi wote wamepelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
Comments