Skip to main content

Shaka ataja kila kitu walivyomtumbua Jokate

Shaka ataja Sababu za Jokate kutenguliwa katika nafasi Yake.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ndugu  Shaka Hamdu Shaka amesema kutenguliwa kwa uteuzi wa Kaimu Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi jumuiya hiyo, Jokate Mwegelo ni maazimio yaliyoridhiwa na Baraza Kuu la Jumuiya hiyo.

Uamuzi wa kutenguliwa kwa uteuzi huo wa Jokate Mwegelo, umetangazwa Leo na Mwenyekiti wa UVCCM,  Ndugu Kheri James mjini Dodoma Leo Jumapili Machi 25 2018, Kufunga Kikao cha Baraza Kuu la jumuiya hiyo, iliyotanguliwa na semina elekezi huku akisisitiza nafasi hiyo itajazwa baadaye.

Akizungumza Ndugu Shaka amesema sababu za kutenguliwa kwa Jokate inatokana na uamuzi wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja huo iliyokutana kwa dharura Leo mchana chini ya Mwenyekiti wake, Ndugu  Kheri James na kuazimia kwa pamoja ambapo hatua hiyo ni utaratibu wa kawaida wa vikao vya baraza hilo ambapo ajenda inapowasilishwa bila kujali aliyewasilisha ni nani na kikao kinaporidhia inakuwa ni ajenda ya kikao.

“Itoshe tu kusema ni utaratibu wa kawaida ndani ya CCM pamoja na jumuiya zake kufanya mabadiliko ya aina yoyote pale wanapoona inafaa,” amesema shaka kwa kifupi.

Jokate ametumikia nafasi hiyo kwa miezi 11 tangu ateuliwe Aprili 24, mwaka jana.

Comments

Popular posts from this blog

DAWA YA ASILI NA USAFI KWA WANAWAKE NI MUHIMU

Dawa ya Uchafu Ukeni Kwa kawaida mwanamke hutokwa na majimaji mepesi (vaginal fluids) yenye rangi nyeupe au ya njano. Inapotokea anatokwa na majimaji yenye ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali na muwasho, hiyo huwa ni ishara ya ugonjwa uitwao wa kutokwa uchafu ukeni ujulikanao kwa kitaalamu kama ‘Vaginosis’. Mwanamke mwenye tatizo hili hujisikia vibaya na anaweza akaacha kushiriki tendo la ndoa ama kwa kuhofia maumivu au kwa kuona aibu kwani mwanaume ni vigumu kuvumilia harufu hiyo au hata kuuona tu huo ute ute kwani humjengea hisia kwamba mwenza wake atakuwa na magonjwa ya zinaa au si mwaminifu kwa ujumla. Kinachosababisha kutokwa na uchafu ukeni: • Kuwa na wapenzi wengi • Baadhi ya dawa za uzazi wa mpango • Kusafisha uke kwa kutumia dawa zenye kemikali • Uchafu • Uvutaji sigara • Pombe • Maambukizi ya Bakteria au bakteria wabaya wanapozidi ukeni Dalili: • Kutokwa na uchafu us...

FAIDA ZA MAZIWA YA SOYA MWILINI

DONDOO ZA AFYA........!!!! MAAJABU YA SOYA MWILINI. MAAJABU YA SOYA MWILINI. Soya ni zao la jamii ya mikunde lenye aina nyingi za matumizi; ni zao linalofaa kwa chakula cha binadamu na wanyama na pia ni zao la biashara. Zao hilo lina kiasi kingi cha protini yenye ubora wa hali ya juu kuliko kiasi kilichopo katika aina nyingine ya mazao ya mimea.ZK  taasisi inayojishughuliza na uzalishaji wa bidhaa za vyakula lishe na mimea na matunda, vinavyoweza kutiba magonjwa mbalimbali wamezalisha maziwa ya Soya ambayo yana  kiasi cha protini inayozidi hata kiasi cha protini katika nyama, mayai na maziwa. Hii inamaanisha kuwa maziwa ya soya ni chanzo rahisi na cha bei nafuu cha protini hasa kwa watu wenye kipato kidogo ambao hawawezi kumudu gharama za vyanzo vingine vya protini kama nyama, maziwa na samaki. Aidha, maziwa ya soya yanaa mafuta bora yasiyo kuwa na lehemu (cholesterol). Uwingi na ubora wa protini katika maziwa ya soya yanaweza kuondoa utapiamlo hususani kwa watoto na kuwao...

The court system during colonialism in Tanzania.

Introduction. Pre-colonial Period Administration of justice during this time depended heavily on the social economic and political organization of the society in Tanganyika. Two systems of administration of justice namely; The Centralized and the Non-Centralized systems could be identified at the time. The Centralized Systems was applicable to societies with chiefs who played both roles of adjudicators and that of governors. In the Non-Centralized systems the entire community took part in the adjudication of disputes. However in both systems there were no formalization of procedure in adjudication, the customs of the respective societies prevailed in the process. Colonial Period The German Colonial Period. The Land currently covering Tanzania Main Land, was then included in what was called the German East Africa, it was subjected to the German Colonial Rule from 1886 up to the end of the First Ward War, 1918. During this Germany Colonial Rule the Administration of Justi...