MSANII BABA REVO AMBAYE NI DIWANI AMPIGA DAKTARI KISA KUCHELEWA KUWALIPA VIBARUA
Diwani wa Kata ya Mwanga Kaskazini Mkoani Kigoma Revokatus Kipando maarufu kwa jina la Baba Levo amemdhalilisha kwa kumpiga Dk. wa Zahanati ya Msufini iliyoko mkoani kigoma kwa kosa la kuchelewesha kuwalipa vibarua waliokua wanafanya ukarabati katika zahanati hiyo.
Daktari huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema diwani alifika nakuanza kumdhalilisha na kumkashifu kwa kuchelewesha kuwalipa wafanyakazi hao mbele ya wagonjwa na kusababisha wagojwa kuondoka pasipo kutibiwa.
“Amefika hapa kwa kufoka, kunitukana , kufanya vurugu ofisini na kanipiga, kisa pesa zilizo nje ya uwezo wangu ambazo zilikua na utaratibu za kufuatiliwa lakini hataki kufuata taratibu za kazi amehatalisha amani ya maisha yangu na hii siyo mara ya kwanza na yuko kinyume cha sheria,” alisema Daktari huyo.
Kwa mjibu wa mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Muuguzi wa Hospitali wa zamu ambaye jina lake limehifadhiwa alisema Diwani huyo malufu kama baba alifika katika zahanati hiyo na kuanza kumfokea Daktari huyo kisha kumpiga.
Kwa upande wake Diwani huyo wa Mwanga Kasikazini maarufu kama Baba Levo amekana kufanya kitendo hicho cha udhalilishaji kwa Daktari mpaka sasa Jshi la Polisi mkoani Kigoma linamsaka mtuhumiwa huyo ili kujibu mashitaka yanayo mkabili.
Comments