Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amekabidhiwa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi Million 400 kutoka kiwanda cha MMI Steel ltd kwaajili ya kampeni ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu Dar es salaam.
Vifaa alivyokabidhiwa ni Mabati 15,000 yenye thamani ya shilingi Million 360, Nondo Tani 22 zenye thamani ya million 40 ambapo kiwanda hicho kimemuahidi tena kumpatia RC Makonda vifaa vingine ikiwemo Rangi, Nondo na Mabati.
Akipokea vifaa hivyo RC Makonda ameshukuru kiwanda cha MMI Steel chini ya mkurugenzi wake Subhash Patel kwa kuwa mdau mkubwa wa kampeni ya ujenzi wa ofisi za walimu na kuwasihi wadau na wananchi kujitokeza kuchangia kampeni hiyo ili kutoa heshima kwa walimu.
Aidha RC Makonda amesema kampeni ya ujezi wa ofisi za walimu inaendelea vizuri ambapo hivi karibuni atapokea kontena nyingine 16 za furniture kutoka Marekani, Kontena 10 za Vitabu kwaajili ya Maktaba ya jamii kutoka Marekani, Kontena 10 za vifaa tiba kutoka uingereza na kontena 10 za Maziwa kutoka China kwaajili ya watoto waliojitokeza wakati wa Zoezi la kutafuta haki ya watoto waliotelekeza Kama sehemu ya msaada.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kiwanda cha MMI Steel Ltd Bwana Subhash Patel amesema wameamua kutoa vifaa hivyo kama sehemu ya kutambua umuhimu wa elimu na kuunga mkono jitihada za RC Makonda katika uboreahaji wa elimu kupitia mazingira bora ya walimu kufanya kazi.
Comments