Skip to main content

ACACIA:BAADA YA MARUFUKU YA MAKINIKIA WAAMUA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MAREKANI

Ni baada ya kupatwa na pigo kubwa

Baada ya Serikali ya Tanzania kuweka zuio la kutosafirisha Makinikia Kampuni  ya Acacia, jana ilitangaza kufungua 'kesi' ya kuomba upatanishi wa mgogoro unaoendelea baina yake na serikali.

Taarifa iliyotolewa jana na Acacia ilisema kampuni hiyo imewasilisha taarifa hiyo ya kutafuta upatanishi kwa niaba ya kampuni zake tanzu za Bulyanhulu Gold Mine Limited (BGML) na Pangea Minerals Limited (PML), inayomiliki mgodi wa Buzwagi.

Kampuni hiyo ya Uingereza inamiliki pia mgodi wa dhahabu wa North Mara, lakini ni miwili hiyo ambayo mali yake huhusisha uchenjuaji wa makinikia.

Migogoro ya kimataifa ya kiuwekezaji hutatuliwa na ama Kituo cha Kimataifa cha Utatuzi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) au Chemba ya Kimataifa ya Biashara (ICC).

Ingawa taarifa ya Acacia haikueleza imefungua wapi ombi lake la kutaka upatanishi wa mgogoro wa makinikia, chanzo cha kuaminika kiliiambia pande hizo mbili zitaketishwa pamoja ICSID yenye makao yake makuu Washington DC, Marekani.

"Taarifa za kusudio hili zinahusu mgogoro wa sasa kati ya Serikali ya Tanzania na kila moja kati ya BGML na PML kusuluhishwa," ilisema Acacia katika taarifa yake iliyowekwa kwenye tovuti yake na kuongeza:

"Hii ni kuendana na mchakato wa utatuzi wa migogoro uliokubaliwa na Serikali ya Tanzania katika Makubaliano ya Uendelezaji Madini na BGML and PML.

"Uwasilishaji wa taarifa ya kutafuta upatanishi kwa wakati huu ni muhimu kwa ajili ya kuilinda kampuni. Pamoja na hatua hii, Acacia bado ina mtazamo kuwa mazungumzo nje ya vyombo rasmi ndiyo njia bora ya utatuzi wa migogoro iliyopo na kampuni itaendelea kufanya jitihada kufanikisha hili."

Acacia ilisema serikali pia imeiarifu Barrick, kampuni yake mama, kuwa kwa sasa ingependa kuendelea na mazungumzo yao, hivyo, "Acacia haitashiriki moja kwa moja kwenye mazungumzo hayo yatakapoanza."

"Suluhusho lolote litakaloweza kubainishwa kutokana na mazungumzo hayo litalazimika kupitishwa na Acacia, na kampuni itashirikiana na Barrick kwa hali na mali kusapoti mazungumzo hayo.

KULIPA FEDHA
Juni 14, Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation ya Canada ambayo ni mmiliki mkubwa wa Acacia, Prof. John Thornton alifanya mazungumzo na Rais John Magufuli na kukubali kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na udanganyifu ambao umegundulika kwenye biashara ya makinikia nchini.

Mazungumzo hayo yalifanyika ikiwa zimepita siku tatu tangu Rais akabidhiwe ripoti ya kamati maalum ya pili iliyochunguza masuala ya sheria na kiuchumi kuhusiana na mchanga wa madini unaosafirishwa nje ya nchi.

Ripoti iliyowasilishwa na mwenyekiti Prof. Nehemia Osoro, ilisema nchi inaweza kuwa imepoteza mpaka Sh. trilioni 489 katika kodi na mali (madini) kwa miaka 19 iliyopita kwenye biashara hiyo ya madini inayofanywa na Acacia.
Kati ya fedha hizo, kiwango cha kodi kilitajwa kuwa Sh. trilioni 108.

Taarifa ya Ikulu ilisema baada ya mazungumzo hayo, Prof. Thornton alisema kuwa kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na kwamba ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania.

Acacia imejikuta katika wakati mgumu baada ya kamati ya kwanza iliyoteuliwa na Rais Magufuli Machi 29, ikiwa na wajumbe nane wenye taaluma za jiolojia, kemia, uhandisi kemikali na uhandisi uchenjuaji madini, kuchunguza kiwango cha madini kwenye makontena yenye makinikia kuonyesha kuwapo kwa udanganyifu.

Acacia ndiyo msafirishaji mkuu wa makinikia nchini.

Kamati hiyo maalumu ilikuwa chini ya uenyekiti wa Profesa wa masuala ya miamba, Abdulkarim Mruma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Baada ya kamati ya kwanza kumkabidhi ripoti ya uchunguzi Mei 24, Rais Magufuli alichukua uamuzi wa kusitisha upelekaji mchanga nje ya nchi mpaka itakapoelezwa vinginevyo baadaye.

Na baada ya Kamati ya pili ya Rais kuchunguza masuala ya kisheria na kiuchumi kuhusiana na makinikia yanayosafirishwa nje ya nchi tangu mwaka 1998 kugundua Acacia haijasajiliwa kwa mujibu wa sheria, Rais Magufuli alisitisha moja kwa moja usafirishaji huo.

Comments

Popular posts from this blog

DAWA YA ASILI NA USAFI KWA WANAWAKE NI MUHIMU

Dawa ya Uchafu Ukeni Kwa kawaida mwanamke hutokwa na majimaji mepesi (vaginal fluids) yenye rangi nyeupe au ya njano. Inapotokea anatokwa na majimaji yenye ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali na muwasho, hiyo huwa ni ishara ya ugonjwa uitwao wa kutokwa uchafu ukeni ujulikanao kwa kitaalamu kama ‘Vaginosis’. Mwanamke mwenye tatizo hili hujisikia vibaya na anaweza akaacha kushiriki tendo la ndoa ama kwa kuhofia maumivu au kwa kuona aibu kwani mwanaume ni vigumu kuvumilia harufu hiyo au hata kuuona tu huo ute ute kwani humjengea hisia kwamba mwenza wake atakuwa na magonjwa ya zinaa au si mwaminifu kwa ujumla. Kinachosababisha kutokwa na uchafu ukeni: • Kuwa na wapenzi wengi • Baadhi ya dawa za uzazi wa mpango • Kusafisha uke kwa kutumia dawa zenye kemikali • Uchafu • Uvutaji sigara • Pombe • Maambukizi ya Bakteria au bakteria wabaya wanapozidi ukeni Dalili: • Kutokwa na uchafu us...

FAIDA ZA MAZIWA YA SOYA MWILINI

DONDOO ZA AFYA........!!!! MAAJABU YA SOYA MWILINI. MAAJABU YA SOYA MWILINI. Soya ni zao la jamii ya mikunde lenye aina nyingi za matumizi; ni zao linalofaa kwa chakula cha binadamu na wanyama na pia ni zao la biashara. Zao hilo lina kiasi kingi cha protini yenye ubora wa hali ya juu kuliko kiasi kilichopo katika aina nyingine ya mazao ya mimea.ZK  taasisi inayojishughuliza na uzalishaji wa bidhaa za vyakula lishe na mimea na matunda, vinavyoweza kutiba magonjwa mbalimbali wamezalisha maziwa ya Soya ambayo yana  kiasi cha protini inayozidi hata kiasi cha protini katika nyama, mayai na maziwa. Hii inamaanisha kuwa maziwa ya soya ni chanzo rahisi na cha bei nafuu cha protini hasa kwa watu wenye kipato kidogo ambao hawawezi kumudu gharama za vyanzo vingine vya protini kama nyama, maziwa na samaki. Aidha, maziwa ya soya yanaa mafuta bora yasiyo kuwa na lehemu (cholesterol). Uwingi na ubora wa protini katika maziwa ya soya yanaweza kuondoa utapiamlo hususani kwa watoto na kuwao...

FAIDA 30 ZA ALOE VERA MWILINI

FAIDA ZA MMEA WA ALOE VERA (Mshubiri): Mshubiri ni mti wenye Miujiza ya kutibu maradhi sugu kama ugonjwa wa Saratani (Cancer) ugonjwa wa Kisukari Diabetis, Ugonjwa wa cholesterol, ugonjwa wa kuvimba sehemu ya mwili na magonjwa mengine mengi. Tuone faida za mmea wa aloe vera au mshubiri 1. Huondoa uvimbe katika jicho Weka kiasi kidogo cha majimaji ya mu-aloe vera freshi kisha kuamka asubuhi, acha kwa dakika kadhaa kisha jisafishe. Uvimbe lazima ukimbie. Pia unaweza kuloweka pamba katika majimaji ya mualoe vera na kisha jisafishe katika jicho lenye uvimbe. 2. Huzuia na kuondoa michirizi ya tumbo itokanayo na ujauzito Anza kwa kupakaa majimaji ya mualoevera juu ya tumbo lako na ufanye kama masaji hivi taratibu juu ya tumbo mara 2 kwa siku katika kipindi chote cha ujauzito na baada ya kujifungua kwa miezi michache mpaka michirizi ipotee yote. 3. Hutibu bawasiri Ile ile sifa moja iliyonayo ya kutibu uvimbe ambayo inaweza pia kutibu malengelenge na uvimbeuchungu kwenye mwako wa mwili...