SHAKA: TUNDU LISSU AMECHOKA MAISHA YA URAIANI
"Tumemtafakari na kubaini ana nia ya kuwania urais mwaka 2020, anachotaka ni kuwaacha kwenye mataa jamaa zake kina Lowasa na sumaye, ila ajue akizidi kueneza matamshi ya kipuuzi anaweza kukamatwa na kutupwa mahali" - Shaka
"Lisu si kama papai ambalo kama likiwekwa ndani litaooza na kuharibika, anaweza kukaa huko kwa usalama wake na wa nchi, tumeruhusiwa kisheria kufanya siasa za vyama vingi kwa ustaarabu na uungwana na si kufanyiana kejeli na dhihaka " - Shaka
"Lisu ni nani mbele ya mamlaka za kisheria na kikatiba, tunadhani anataka nyingi nasaba hivyo ajiandae siku yoyote anaweza kukutwa na msiba, msiba wa kujitakia hauna pole, dola yoyote haifanani na kitambaa cha deki" - Shaka
"Ujasiri wa kuidhihaki mamlaka ya Rais ni sawa na mtu juha au punguani anayejaribu kutupa jiwe katikati ya mzinga wa nyuki au mpumbavu kumchezea simba sharubu " - Shaka
Shaka H. Shaka ni Kaimu Katibu Mkuu UVCCM
Comments