Hashim Rungwe amshauri Tundu Lissu kumpuuza Zitto Kabwe
Mwenyekiti wa chama cha Sauti ya UMMA Hashim Rungwe amemuomba Rais wa Chama cha Sheria Tanganyika Tundu Lissu kumpuuza Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.
Rungwe amesema alishangazwa na kejeli alizomwaga Zitto Kabwe dhidi ya Lissu ambaye kwa sasa ndiye mwanasiasa tishio zaidi nchini.
Rungwe amesema Zitto kama alikuwa anapinga msimamo wa Chadema angepaswa kutoa hoja na siyo mipasho aliyotoa.
Kiongozi huyo aliyegombea Urais mwaka 2015 amesema alichokisema Tundu Lissu ndiyo msimamo wa mpinzani yeyote wa kweli nchini.Amesema na ndiyo sababu CCM wote wamemshangilia Zitto na sasa wanamuona ni mwenzao.
Rungwe amemshauri Tundu Lissu kumpuuza Zitto Kabwe kwani kujibizana naye inaweza kuwa mkakati wa CCM wa kupunguza mashambulizi dhidi yake.
Rungwe amemalizia kwa kusema nchi nyingi za Afrika watawala wamepandikiza wapinzani bandia na vibaraka ili kutawala muda mrefu.
Comments