HUSSEIN BASHE ASHANGAA MCHANGA KUWAPA HASARA ACACIA.
"Mheshimiwa Rais, naomba nikupe taarifa - tarehe 21 Julai, Mkurugenzi Mtendaji wa ACACIA ametangaza kuwa shareholders wa ACACIA hawatawalipwa gawio kwa sababu cashflow yao imepungua kwa asilimia 80% kufuatia uamuzi wako wa kuzuia makontena ya makinikia. Hivyo hawatalipwa hadi ufumbuzi wa makontena hayo utakapopatikana.
"Sasa najiuliza mbona walisema ule mchanga tu na wala hauna thamani?
Sasa iweje leo makapi yawe na thamani ya asilimia 80% kiasi cha kufanya shareholders wakose gawio?"
Mh Hussein Bashe
Mbunge - Nzega Mjini (CCM)
(akiongea kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli mkoani Tabora)
Comments