Kijana wa miaka 22 na mhitimu wa chuo cha Abia State Nigeria faculty ya Historia alikamatwa Jana mchana akiwa anambaka msichana wa miaka 10.
Kijana huyu kabla hajafanya kitendo hicho, mnamo mda wa saa 8 mchana alipita nyumbani kwa baba yake na kumsalimia na kuulizia kuhusu biashara za baba yake zinaendaje, kisha akaondoka kuelekea kwake, kabla hajafika kwake alipita nyumbani kwa msichana yule aliyebakwa na kumsalimia...........
Baba wa kijana huyu ni Fundi wa kutengeneza Samani za ndani.
Kijana huyu alimwambia msichana yule kuwa amemnunulia kandambili mpya kisha akamwambia waende wote chumbani kwake ili akampatie, na walipofika hakumpatia kqnfambili hizo alianza kumshikashika msichana yule kwenye mwili wake na kisha kuanza kumlazimisha kufanya tendo la ngono bila ridhaa yake.
Mtuhumiwa alikamatwa na vijana majirani zake waliosikia kelele za msichana yule.
Kijana huyu wa miaka 22 akithibitisha kufanya kitendo hicho kiovu alisema ni kweli alimbaka msichana yule. Katika upelelezi iligundulika kuwa hata hizo kandambili zilikuwa za dada yake mwenye umri wa miaka 18.
Baba wa kijana huyu alipohojiwa alisema alikuwa nyumbani kisha akapigiwa simu ya ghafla na kuambiwa kuwa kijana wake amemlawiti msichana wa miaka 10 huko chuoni Abia State huku akilalamika kuwa sio yeye aliyefanya kitendo hicho ila ni shetani tu ndie aliyemsukuma na kufanya kitendo hicho.
Endelea kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii
Facebook Reuben Paul
Twitter Reuben Paul
Instagram reuben_tv au Reuben.com
YouTube Reuben Tv
Comments