Skip to main content

RC PAUL MAKONDA AZAWADIWA GARI NA KAMPUNI YA UTENGENEZAJI WA MAGARI

RC MAKONDA AKABIDHIWA WINGLE 5

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mh. Paul Makonda leo asubuhi amekabidhiwa zawadi ya gari aina ya *Double Cabin Wingle 5 kutoka kwa kampuni ya watengenezaji wa magari ya  *Great Wall Motor Company* ya Afrika Kusini ikishirikiana na kampuni ya wauzaji Magari ya *Kifaru Motors* ya Tanzania.

Akiongea katika makabidhiano hayo mkurugenzi wa *Great Wall Motor Company* ukanda wa Kusini mwa Afrika *Bwana Jianguo Liu* alisema kuwa zawadi hiyo ni ishara ya kampuni hiyo kutambua jitihada mbalimbali  za ofisi ya mkuu wa Mkoa na watumishi wake wanazofanya katika kutumikia wananchi na kusaidia kuboresha utendaji kazi.

Katika salamu za shukrani *Mh. Makonda* alishukuru uongozi mzima wa kampuni ya *Great Wall* ukishirikiana na wauzaji *Kifaru Motors* kwa kutambua jitihada za ofisi yake na kuahidi kuendelea kuwatumikia wananchi wa Dar es salaam kwa moyo na kutimiza falsafa ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania *Mh. Dr John Pombe Magufuli* ya *"HAPA KAZI TU"*.

Mkuu wa Mkoa ameahidi kuwa gari hilo litatumika ipasavyo katika kuwahudumia wananchi wa Dar es salaam kutumia idara itakayoonekana kuwa ndio Mtoa huduma bora katika Mkoa wa Dar es salaam.

*"Naomba kuitoa hii gari kama Zawadi kwa Idara inayohudumia vizuri wananchi wangu na ili nitoe kwa idara hiyo naomba wananchi wenyewe watutumie kwa ujumbe mfupi kupitia namba tutakayoitangaza . Kazi ya mwananchi ni kusema tu idara hii inawahudumia vizuri wanapofika kwenye ofisi zao, kama ni Afya,elimu,Ardhi,Biashara na Mahakama."* Aliongeza *Makonda.*

Kwa mfano kama ulienda idara ya Elimu, Ardhi, Afya au Biashara ukapewa huduma nzuri katika eneo mojawapo kati ya hayo unachotakiwa ni kutuma meseji fupi inayoonyesha idara hiyo ili wapewe zawadi hiyo ya Gari kama motisha waendelee kutoa huduma nzuri.

Utaratibu wa kutuma ujumbe huo wa kuchagua idara bora katika utendaji utatolewa kupitia namba maalum ambayo itatolewa hapo baade.

Comments

Popular posts from this blog

The court system during colonialism in Tanzania.

Introduction. Pre-colonial Period Administration of justice during this time depended heavily on the social economic and political organization of the society in Tanganyika. Two systems of administration of justice namely; The Centralized and the Non-Centralized systems could be identified at the time. The Centralized Systems was applicable to societies with chiefs who played both roles of adjudicators and that of governors. In the Non-Centralized systems the entire community took part in the adjudication of disputes. However in both systems there were no formalization of procedure in adjudication, the customs of the respective societies prevailed in the process. Colonial Period The German Colonial Period. The Land currently covering Tanzania Main Land, was then included in what was called the German East Africa, it was subjected to the German Colonial Rule from 1886 up to the end of the First Ward War, 1918. During this Germany Colonial Rule the Administration of Justi...

Ndege ya Ukraine yaanguka Iran ikiwa na abiria 180, Abiria wote wafariki

Ndege ya Ukraine aina ya Boeing-737 iliyokuwa na abiria 180 imeanguka Iran, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo. Watoa huduma wa msalaba mwekundu wa Iran wanasema kuwa hakuna dalili yeyote kama kuna mtu aliyepona katika ajali hiyo. Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la kimataifa la ndege la Ukraine ilianguka muda mfupi baada ya kuanza safari katika uwanja wa ndege wa Imam Khomeini mjini Tehran. Ripoti za awali zinadai kuwa ndege hiyo ilikuwa safarini kuelekea mji mkuu wa Ukraine, Kyiv.  Haijabainika ikiwa ajali hiyo ina uhusiano wowote na mzozo wa Iran-na Marekani. Kikosi cha uokoaji tayari kimetumwa katika eneo la tukio karibu na uwanja wa ndege, eneo ambalo ndege lilianguka. Credit: GettyImage " Ndege imeshika moto na tumetuma kikosi huko ... ," kiongozi wa huduma za dharura Pirhossein Koulivand,ameviambia vyombo vya habari ambapo Reuters imeripoti. Je tutegemee machafuko zaidi kutokea? Endelea kuwa pamoja nasi bega kwa bega, mshirikishe na mwenz...