Figo zina majukumu muhimu sana katika
mwili wa binadamu- kwanza inaondoa
sumu kutoka mwili wa binadamu na
kusafisha damu na kutoa sumu zote.
Kama figo haifanyi kazi vizuri, basi hii
inaweza kusababisha mkusanyiko wa
sumu katika mwili na inaweza kusababisha baadhi ya matatizo
makubwa ya afya.
Dalili za mwanzo za ugonjwa wa figo na
jinsi ya kuweka figo zako katika afya
nzuri.
Figo inafanya kazi nyingi muhimu katika
mwili wa binadamu.
1.Kuweka katika uwiano mzuri kiwango
cha maji.
Figo ina uwezo wa kusawazisha kiwango
cha maji katika mwili wa binadamu,na
pia inashiriki katika kutoa kemikali kwa
njia ya mkojo.
2.Kutoa taka mwilini.
Sisi sote tunajua moja ya kazi kuu za figo
ni kusafisha mwili, kutoa sumu,chumvi
na urea.
3.Kusimamia kanuni za damu.
Kama kiwango cha oksijeni kitakuwa
chini katika figo, itasababisha kuundwa
kwa erythroprotein, homoni ambayo
inachochea marrow katika mifupa(bone
marrow).
4.Kusimamia Kanuni za asidi.
Hii ni muhimu sana katika kazi za figo,
figo zinawajibika kwa kuweka uwiano
sawa wa asidi katika mwili wa binadamu
MAGONJWA YA FIGO.
Kuna sababu nyingi tofauti zinazoweza
kukusababishia ugonjwa wa figo na
kushindwa kufanya kazi, magonjwa
kama kisukari,ukimwi na shinikizo la
damu.
Tunaweza kusema shinikizo la damu ni
moja ya sababu ya ugonjwa wa figo na
hii ndio maana inapaswa kujaribu
kuweka sukari katika damu na BP katika
uwiano wa kawaida.
Dalili za mwanzo za ugonjwa wa
figo zinaanza kuonekana katika hatua za
mwisho za ugonjwa,au wakati figo
zinakaribia kabisa kushindwa au wakati
ambao kuna protini nyingi katika mkojo.
Kwa kawaida dalili za awali za matatizo
ya figo haziwezi kugundulika, ni asilimia
10 tu ya watu wanaweza kujua kama wana ugonjwa wa figo.
Hizi ni baadhi ya ishara za mwanzo za
figo kushindwa kufanya kazi.
-Kubadilika rangi kwa mkojo(mfano
damu katika mkojo au kwenda haja
ndogo mara kwa mara).
-Uchovu na kukosa nguvu.
-Maumivu ya mgongo hasa juu ya kiuno
usawa wa figo.
-Kuvimba miguu au mikono.
-Ukosefu wa umakini na ufafanuzi wa
akili.
-Kukosa hamu ya kula na kutokuwa na
ladha katika kinywa.
-Kushindwa kupumua vizuri.
-Upele au chronic tingling
Jinsi ya kuzuia ugonjwa wa figo na
kuboresha kazi ya figo yako.
Kama tulivyosema awali,magonjwa ya
figo yanaweza kukuletea matatizo
makubwa zaidi katika afya zetu.
Inatupasa kufanya mabadiliko katika
milo yetu na maisha kwa ujumla
-Kipi cha kubadilisha katika mlo.
Chakula chako kisiwe na mafuta mengi,
zuia utumiaji kupita kiasi wa chumvi na
potassium, na upendelee kula matikiti
maji au apples na katika chakula chako
kiwe na kiwango kidogo cha protein. Na
pia matumizi ya maji yawe si chini ya
glasi nane kila siku
-Mfumo wa maisha Pendelea kufanya mazoezi hili kuweka uzito wako vizuri na kupunguza uwezekano wa kupata kisukari,na utapiamlo. Na pia zuia matumizi ya pombe na kuacha sigara.
Comments