Rais John Magufuli amesema amepata mialiko zaidi ya 60 kwenda nje ya nchi baada ya kuwa Rais lakini ameikataa kwa sababu anataka kuishughulikia Tanzania kwanza.
“Niende nje kufanya nini wakati ntaenda tu nikishastaafu, nataka nimalize kwanza haya ya hapa ndani,” alisema.
Ameyasema hayo jana (Jumanne Julai 4) wakati akihutubia wakazi wa Sengerema katika uzinduzi wa mradi wa maji Sengerema.
Rais Magufuli amesema hana haja ya kwenda nje ya nchi kwa sababu bado ana mzigo mkubwa wa kumaliza ufisadi.
Comments