Putin aagiza wanadiplomasia 755 wa Marekani kuondoka Urusi
Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter
HakiAFPImageKufukuzwa wa wanadiplomasia hao kutapunguza idadi hadi 455
Rais wa Urusi Vladimir Putin ameagiza wafanyakazi 755 wa ubalozi wa Marekani nchini Urusi kusitisha shughuli zao kufikia Septemba mosi mwaka huu.
Urusi imeidhinisha hatua hiyo kwa ghadhabu kufuatia vikwazo vipya vilivyopitishwa na bunge la Marekani dhidi yake, kwa tuhuma za kuingilia uchaguzi wa taifa hilo mwaka jana.
Marekani kwa upande wake, inasema imesikitishwa na uamuzi huo, na inapima athari na kutafakari namna ya kujibu hatua hiyo
Marekani yawafukuza wanadiplomasia 35 wa UrusiBunge la wawakilishi Marekani launga mkono vikwazo dhidi ya Urusi
Hatua hii ya Urusi imekuja baada ya vikwazo vipya dhidi ya Urusi kuidhinishwa kwa wingi wa kura na mabunge yote ya congress nchini Marekani Jumanne, licha ya kwamba Ikulu ya White house ilipinga kura hiyo.
Rais huyo wa Urusi ameapa kuwa upo uwezekano wa kuongeza vikwazo zaidi dhidi ya serikali ya Marekani.
HakiEPAImageUrusi imewapiga wanadiplomasia wa Marekani
Akizungumza kwenye televisheni ya taifa ya Urusi, rais Putin alisema kuwa alitarajia uhusiano baina ya Moscow na Washington ungebadilika na kuwa mzuri, lakini hilo haliwezekani kwa sasa.
Akizungumza na wakati wa ziara yake nchini Estonia, makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence, alisema anatumai kwamba mienendo ya serikali ya Urusi itabadilika.
Trump na Merkel wasema walidukuliwa na ObamaUrusi yawafukuza wanadiplomasia wa Moldova
Mashirika ya ujasusi nchini Marekani yanaamini kuwa Urusi ilijaribu kuingilia uchaguzi wa urais wa mwaka 2016 kwa lengo la kumsaidia Donald Trump kupata ushindi.
Urusi imekuwa ikikanusha kuingilia kwa vyovyote uchaguzi huo.
HakiEPAImageUrusi inalitwaa ghala hili la Marekani lililo Moscow
Comments