UJUE UGONJWA WA
(hemorrhoid) kuota kinyama sehemu ya haja kubwa.
Maada hii ni muhimu sana maana ni tatizo linalowatesa watu wengi ungana nami hapa uweze kupata elimu pia .
Bawasirini (kuota kinyama sehemu ya haja kubwa) ni uvimbe wa mishipa ya damu kwenye njia ya haja kubwa. Huonekana kutuna au kujaa kama jipu karibu na unyeo. Inaweza kutoa muwasho, hisia ya kuungua, au maumivu; hasa wakati wa kujisaidia. Wakati mwingine bawasiri hupasuka na kutoa damu kidogo nyekundu inayong’aa kwenye kinyesi.
Bawasiri ni tatizo la kawaida wakati wa ujauzito na miongoni mwa watu wanaokaa au kubeba mizigo mikubwa kutwa nzima, lakini kila mtu anaweza kuupata. Maumivu kutokana na bawasiri huzidi zaidi mgonjwa anapokuwa na tatizo la choo kigumu, kwa sababu kukitoa choo kigumu hulazimisha mishipa kwenye njia ya haja kubwa kupanuka zaidi.
bawasiri zipo za aina mbili.
1 Aina inayotembea (Yaani ikitoka ndani na kurudi)
2 Aina inayosimama
VISABABISHI VYA BAWASIRI (KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA)
Kisababishi kamili cha bawasiri hakijulikani. Baadhi ya vipengele vichangiapo ni pamoja na: Mazoea ya utumbo yasiyojirudia (kufungika kwa choo au kuhara), ukosefu wa mazoezi, visababishi vya lishe (chakula kilicho na kiwango cha chini cha faiba), ongezeko la shinikizo la ndani la fumbatio (uchovu unaoendelea kwa muda, asitisi, ukubwa wa ndani wa fumbatio, au ujauzito), jenetiki, kutokuwepo kwa vali katika vena ya hemoroidi, na kuongezeka kwa umri.
Visababishi vingine vinayoaminiwa kuongeza hatari ni pamoja na unene, kuketi chini kwa muda mrefu,[2] kikohozi kinachoendelea kwa muda na sakafu ya pelvisi kutofanya kazi.
JINSI YA KUEPUKANA NA HILI TATIZO LA BAWASIRI
•Epuka tatizo la ugumu wa choo na bawasiri kwa kujenga tabia ya kunywa maji mengi, kula matunda kwa wingi na nafaka nzimanzima ambazo hazijasindikwa.
•Baadhi ya juisi kutokana na mimea chungu ikipakwa kwenye bawasiri husaidia uvimbe kunywea.
•Kaa kwenye benseni au bafu yenye maji vuguvugu kusafisha bawasiri na kupunguza maumivu.
•Usifute unyeo kwa kutumia mabunzi, gazeti, au vifaa vingine visivyo laini.
•Badala yake, tumia karatasi maalum ya kutawazia (toilet paper) au chombo cha maji kwa ajili ya kusafisha unyeo baada ya kujisaidia.
TIBA IFUATAYO HUSAIDIA KUPUNGUZA MAUMIVU NA KUONDOA BAWASIRI
UNAWEZA KUTUMIA KIMOJA WAPO
Kitunguu thaumu (Vijiko vitatu vya chakula), Asali (Nusu lita)
Tangawizi (Vijiko vitatu vya chakula)
MATUMIZI: Madawa haya lazima yapimwe kwa idadi hiyo yakiwa tayari yamekuwa unga, kisha changanya pamoja, na dozi yake ni kama ifuatayo; Kijiko kimoja cha unga wa madawa haya utakilamba asubuhi, mchana utafanya kama hivyo tena kisha jioni yaani (1 X 3) kwa muda wa siku saba hadi kumi na moja (7 - 11).
Natumai tumejifunza kitu ili kuweza kuepukana na tatizo Hili...
Na.. Elly Rodgers Masha..
Comments