Skip to main content

NAIBU SPIKA: WAPINZANI HAWAJUI KUZICHANGANUA HOJA LICHA YA UWASILISHAJI WAO MZURI



Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson.

Naibu spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt.  Tulia Ackson  amefunguka na kusema wabunge wa upinzani muda mwingine huwa wanaleta hoja nzuri kwa serikali lakini serikali inashindwa kuzipokea hoja hizo kutokana na uwasilishaji wao.

Naibu Spika amesema hayo leo Dodoma wakati akifanyiwa mahojiano katika kipindi cha bunge, ambapo alikuwa akitoa mtazamo wake juu ya bajeti kuu ya serikali kwa mwaka 2017/2018
"Wabunge wa upinzani muda mwingine wanaleta hoja nzuri sana bungeni lakini tatizo kubwa linakuja katika lugha inayotumika inakuwa si lugha ya staha ndiyo maana unaona hata serikali inakuwa haikubali. Bunge ni jumba la kisiasa, hivyo kila mwamba ngoma huvutia kwake, upande wa chama kinachoongoza ndiyo chenye serikali wana namna yao ya kuishauri serikali, ila wale ambao wanataka kuingia madarakani nao wana namna yao ya uchangiaji bungeni ndiyo maana kuna kuwa na mvutano wa hapa na pale" alisema  Tulia Ackson

Mbali na hilo Naibu Spika alidai serikali muda mwingine imekuwa inashindwa kufanyia kazi kwa haraka baadhi ya ushauri wa wabunge utolewao bungeni kutokana na ukweli kwamba serikali kabla ya kuleta jambo bungeni huwa inakuwa imefanya utafiti wa kutosha, hivyo linapoibuka jambo jipya inakuwa changamoto, inabidi ilichukue na kuja kulifanyia kazi siku za mbeleni.

Kuhusu upendeleo bungeni Naibu Spika amesema wabunge wote wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wapinzani wamekuwa wakipewa nafasi sawa lakini wabunge wa upinzani wamekuwa wakilalamika kutokana na kuwa na dhana ya kuonewa.

"Bunge hili limekuwa na wabunge zaidi ya 300 na walio wengi zaidi ni wabunge kutoka chama tawala, hivyo wale wa upinzani kwa kuwa wapo wachache hivyo wanaweza kuona kama wanaonewa hivi, wanaweza kuona kama hawasikilizwi, wanaona kama hawapewi muda zaidi, lakini unakuta mtu ukiwa kwenye kile kiti unawaza hili na kufanya utende kwa usawa tena kwa kuwasaidia walio wachache ili dhana hiyo isiwepo" alisisitiza Tulia Ackson

Kwa kumalizia  Tulia Ackson  aligusia jambo la mbunge kulishtaki bunge mahakamani na kusema kuwa hakuna mbunge anaweza kulishtaki bunge kama taasisi

"Bunge kama taasisi likifanya jambo huwezi kulipeleka mahakamani, bunge likiwa limefanya maamuzi juu ya jambo fulani na ukaona bunge halijafanya sawa kuna utaratibu wa kibunge lakini huwezi kuchukua maamuzi ya bunge ukapeleka mahakamani, kwa hiyo kuna utaratibu wake, lakini uamuzi wa bunge huwezi kuupeleka mahakamani kikanuni" alimalizia  Tulia Ackson

Comments

Popular posts from this blog

DAWA YA ASILI NA USAFI KWA WANAWAKE NI MUHIMU

Dawa ya Uchafu Ukeni Kwa kawaida mwanamke hutokwa na majimaji mepesi (vaginal fluids) yenye rangi nyeupe au ya njano. Inapotokea anatokwa na majimaji yenye ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali na muwasho, hiyo huwa ni ishara ya ugonjwa uitwao wa kutokwa uchafu ukeni ujulikanao kwa kitaalamu kama ‘Vaginosis’. Mwanamke mwenye tatizo hili hujisikia vibaya na anaweza akaacha kushiriki tendo la ndoa ama kwa kuhofia maumivu au kwa kuona aibu kwani mwanaume ni vigumu kuvumilia harufu hiyo au hata kuuona tu huo ute ute kwani humjengea hisia kwamba mwenza wake atakuwa na magonjwa ya zinaa au si mwaminifu kwa ujumla. Kinachosababisha kutokwa na uchafu ukeni: • Kuwa na wapenzi wengi • Baadhi ya dawa za uzazi wa mpango • Kusafisha uke kwa kutumia dawa zenye kemikali • Uchafu • Uvutaji sigara • Pombe • Maambukizi ya Bakteria au bakteria wabaya wanapozidi ukeni Dalili: • Kutokwa na uchafu us...

FAIDA ZA MAZIWA YA SOYA MWILINI

DONDOO ZA AFYA........!!!! MAAJABU YA SOYA MWILINI. MAAJABU YA SOYA MWILINI. Soya ni zao la jamii ya mikunde lenye aina nyingi za matumizi; ni zao linalofaa kwa chakula cha binadamu na wanyama na pia ni zao la biashara. Zao hilo lina kiasi kingi cha protini yenye ubora wa hali ya juu kuliko kiasi kilichopo katika aina nyingine ya mazao ya mimea.ZK  taasisi inayojishughuliza na uzalishaji wa bidhaa za vyakula lishe na mimea na matunda, vinavyoweza kutiba magonjwa mbalimbali wamezalisha maziwa ya Soya ambayo yana  kiasi cha protini inayozidi hata kiasi cha protini katika nyama, mayai na maziwa. Hii inamaanisha kuwa maziwa ya soya ni chanzo rahisi na cha bei nafuu cha protini hasa kwa watu wenye kipato kidogo ambao hawawezi kumudu gharama za vyanzo vingine vya protini kama nyama, maziwa na samaki. Aidha, maziwa ya soya yanaa mafuta bora yasiyo kuwa na lehemu (cholesterol). Uwingi na ubora wa protini katika maziwa ya soya yanaweza kuondoa utapiamlo hususani kwa watoto na kuwao...

FAIDA 30 ZA ALOE VERA MWILINI

FAIDA ZA MMEA WA ALOE VERA (Mshubiri): Mshubiri ni mti wenye Miujiza ya kutibu maradhi sugu kama ugonjwa wa Saratani (Cancer) ugonjwa wa Kisukari Diabetis, Ugonjwa wa cholesterol, ugonjwa wa kuvimba sehemu ya mwili na magonjwa mengine mengi. Tuone faida za mmea wa aloe vera au mshubiri 1. Huondoa uvimbe katika jicho Weka kiasi kidogo cha majimaji ya mu-aloe vera freshi kisha kuamka asubuhi, acha kwa dakika kadhaa kisha jisafishe. Uvimbe lazima ukimbie. Pia unaweza kuloweka pamba katika majimaji ya mualoe vera na kisha jisafishe katika jicho lenye uvimbe. 2. Huzuia na kuondoa michirizi ya tumbo itokanayo na ujauzito Anza kwa kupakaa majimaji ya mualoevera juu ya tumbo lako na ufanye kama masaji hivi taratibu juu ya tumbo mara 2 kwa siku katika kipindi chote cha ujauzito na baada ya kujifungua kwa miezi michache mpaka michirizi ipotee yote. 3. Hutibu bawasiri Ile ile sifa moja iliyonayo ya kutibu uvimbe ambayo inaweza pia kutibu malengelenge na uvimbeuchungu kwenye mwako wa mwili...