ZITTO KABWE AMJIBU TUNDU LISSU
"Huu ni uhayawani. Hii ni nchi huru. Kukaribisha wageni kuingilia mambo yetu ni upuuzi na umazwazwa. Tupambane ndani kuleta demokrasia. NDANI" - Zitto Kabwe
"Kama hamtaki kuambiwa ukweli shauri yenu. Ni upuuzi mkubwa kutaka nchi ikatiwe misaada. Ni kasumba ya kikoloni. Ni ujinga usiovumilika" - Zitto Kabwe
"Nataka maendeleo ya watu wetu. Uwekezaji kutoka nje na misaada ni sehemu tu ya juhudi. Mwanasiasa anayetaka nchi inyimwe misaada ni muflisi" - Zitto Kabwe
"Napinga ujinga popote. Leo unamkaribisha mgeni akusaidie Kwa kukata misaada. Ukiingia madarakani si utampa dhahabu yote? Kasumba hovyo kbs" - Zitto Kabwe
"Ndio uuze uhuru wa nchi yako? Misaada Kuwa fimbo Kwa nchi zetu ni jambo la kishamba Sana. Misaada ikikatwa anaumia nani? JPM? Lisu?" - Zitto Kabwe
"Hakuna kupingana. Ninapinga ujinga. Siasa za kukatiwa misaada ni siasa za kizamani, ushamba na kasumba ya kutawaliwa" - Zitto kabwe
"Siasa Ni Maendeleo. Lazima tuonyeshe tofauti Kwa wananchi wetu. Kiongozi lazima ujue lipi la kusema wapi" - Zitto kabwe
Comments