👍 MAAMBUKIZI YA NJIA YA MKOJO (URINARY TRACT INFECTIONS -UTIs) Neno U.T.I si geni masikioni mwa wengi, kwani ni wengi leo utawasikia “naumwa U.T.I”. Japo si wote hulitumia kisahihi. Wengine wana tatizo ambalo ni tofauti na U.T.I, lakini anaweza akaenda hata duka la dawa na kuomba apatiwe dawa za U.T.I. Leo nimeona tubadilishane elimu juu ya hili tatizo, angalau kila mmoja awe na uelewa U.T.I ni nini hasa, inasababisha na nini, na ni jinsi gani anaweza kujikinga. U.T.Is, ni kifupisho cha Urinary Tract Infections, ambayo kwa lugha yetu ni maambukizi ya njia ya mkojo. Kama linavyojieleza, kwamba maambukizi ni lazima yawe ni kwenye njia ya mkojo ndipo tunaita ni U.T.I, na si pengine popote. Una uchafu unatoka ukeni, hiyo ni kitu kingine tofauti nk. Tunapozungumzia njia ya mkojo, ni kutoka eneo la nje hadi kwenye kibofu, na kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo. Kama maambukizi yako eneo la kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo(ikihusisha na figo pia), inaitwa Lowe...
Usipitwe na Habari za Kila Kona ya Dunia.