Skip to main content

JE UNALITAMBUA TATIZO LA U.T.I KWA UNDANI ZAIDI?

👍MAAMBUKIZI YA NJIA YA MKOJO (URINARY TRACT INFECTIONS -UTIs)

Neno U.T.I si geni masikioni mwa wengi, kwani ni wengi leo utawasikia “naumwa U.T.I”. Japo si wote hulitumia kisahihi. Wengine wana tatizo ambalo ni tofauti na U.T.I, lakini anaweza akaenda hata duka la dawa na kuomba apatiwe dawa za U.T.I. Leo nimeona tubadilishane elimu juu ya hili tatizo, angalau kila mmoja awe na uelewa U.T.I ni nini hasa, inasababisha na nini, na ni jinsi gani anaweza kujikinga.

U.T.Is, ni kifupisho cha Urinary Tract Infections, ambayo kwa lugha yetu ni maambukizi ya njia ya mkojo. Kama linavyojieleza, kwamba maambukizi ni lazima yawe ni kwenye njia ya mkojo ndipo tunaita ni U.T.I, na si pengine popote. Una uchafu unatoka ukeni, hiyo ni kitu kingine tofauti nk.
Tunapozungumzia njia ya mkojo, ni kutoka eneo la nje hadi kwenye kibofu, na kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo.

Kama maambukizi yako eneo la kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo(ikihusisha na figo pia), inaitwa Lower Urinary Tract Infect. Na ikihusisha eneo la juu ya kibofu, inaitwa Upper Urinary Tract Infection.
Tatizo hili huwapata wote, wanaume na wanawake. Lakini huwapata zaidi wanawake kutokana na tofauti za kimaumbile. Hii ni kwa sababu kuu mbili, i)njia ya haja ndogo ya mwanamke iko jirani zaidi na njia ya haja kubwa ambapo vijidudu vingi visababishao U.T.I ndipo vinapoishi, ii) mrija wa mkojo (urethra) wa mwanamke ni mfupi ukilinganisha na wa mwanaume, hivyo kufanya iwe rahisi kwa maambukizi kufika kwenye kibofu kwa mwanamke kuliko kwa mwanaume.

*Visababishi*

Tatizo hili husababishwa kwa kiasi kikubwa na bacteria ambao makazi yao ya kawaida utumbo mpana, na hivyo huwa wanapatikana pia kwenye haja kubwa, mfano Escherichia coli na wengineo. Pia, linaweza likasababisha na ‘fungus’ na visababishi vingine, japo ni mara chache sana.

*Vihatarishi na Njia ya Maambukizi*

*a)Kwa wanawake*
• Kujamiiana –hii huweza kuamisha bacteria walio kwenye uume moja kwa moja, ama watokanao na maambukizi ya ukeni kuingia moja kwa moja njia ya mkojo
• Kuchezea ama kuchezewa na mikono michafu maeneo ya uke kunaweza kusababisha maambukizi
• Njia mbaya ya kujisafisha baada ya haja kubwa au ndogo inaweza kuhamisha bacteria walio ktk njia ya haja kubwa na kuingia njia ya mkojo
• Matumizi ya pedi za kike zenye kemikali ya kukata harufu ambao huua bacteria wa asili wa eneo la uke na kukaribisha bacteria wanaosababisha maradhi kuzaliana kwa wingi
Vifuatavyo pia vinaweza vikachangia
• Ujauzito –mara nyingi hushusha kinga ya mwili ya mjamzito
• Upungufu wa homon ya ya kike Oestrogen husababisha bacteria wasababishao U.T.I kuzaliana kirahisi

*b)Kwa wanaume*
• Matatizo ya tezi ya kiume(prostate) mabapo husababisha mrija wa mkojo kuziba, ama kutopitisha mkojo vizuri na kuruhusu bacteria kujenga makazi
• Kutotahiriwa, ambapo nyama ya mbele inaweza kuhifadhi bacteria wasababishao U.T.I
• Kujamiiana kinyume cha maumbile huingiza kirahisi bacteria walio njia ya haja kubwa kwenye njia ya mkojo
• Kujamiiana bila kinga na mwanamke ambaye ana maambukizi ukeni
• Kuwa na VVU ambapo hupunguza uwezo wa mwili kupambana na maambukizi
c)Kwa wote
• Kutokunywa maji na vinyaji kwa wingi –kunywa maji mengi husababisha mkojo kuzalishwa kwa wingi, na kukojoa mara kwa mara na hivyo kusafisha njia ya mkojo
• Kuwekewa mirija inayosaidia kutoa mkojo nje inaweza pia kukaribisha maambukizi
• Matatizo ya figo na mengine kwenye njia ya mkojo yanayoweza kuziba njia ya mkojo
• Kisukari ambapo hudhoosha kinga ya mwili na pia kuharibu mfumo wa figo wa uchujaji

*Dalili za U.T.I*
a) Kwa eneo la chini la njia ya mkojo
i. Hali ya kujisikia kutaka kukojoa muda wote
ii. Maumivu, au hali ya kujisikia kuchoma choma wakati wa kukojoa
iii. Kukojoa mara kwa mara na mara zote mkojo ni mdogo
iv. Mkojo unaweza kuonekana una ukungu, na mara nyingine unatoa harufu kali
v. Maumivu ya nyonga kwa wanawake
vi. Maumivu ya rektamu(rectum) kwa wanaume
vii. Na mara nyingine damu kwenye mkojo

b) Kwa eneo la juu la njia ya mkojo
i. Maumivu ya tumbo(hasa eneo la juu kwa pembeni –chini ya mbavu)
ii. Homa kali
iii. Kutetemeka na kujihisi baridi
iv. Kichefuchefu na /au kutapika
Vipimo na matibabu
Mara nyingi kipimo cha mkojo kinaweza kuonyesha tatizo.
Matibabu ni antibiotic baada ya daktari kubaini tatizo

*Madhala yatokanayo na U.T.I*
isipopata tiba sahihi
• Inaweza ikasababisha maambukizi makubwa ya figo(pyenephritis) ambayo yanaweza kusababisha uharibifu wa kudumu wa figo na hivyo kutishia maisha
• Kwa wajawazito inaweza kuhatarisha maisha ya wote mama, na motto aliye tumboni
• Bakteria wanaweza kuingia mfumo wa damu na kusababisha ama kwenda kusababisha madhala mengine
• Inaweza kusababisha shinikizo la damu kuwa kubwa kwenye figo na hata kusababisha ufanyaji wa kazi mbovu wa figo
Tiba mbadala nyumbani kabla ya kumwona daktari
Unaweza kutibu, ama kupunguza tatizo nyumbani kabla ya kumwona daktari pale uonapo dalili ya awali ya U.T.I, ambayo ni maumivu na kuchomachoma wakaji wa kukojoa.

*Fanya yafuatayo*
i. Kunywa maji mengi hasa saa 24 za kwanza baada ya kuona dalili. Hii itasaidia kuzalisha mkojo kwa wingi na kusafisha njia ya mkojo
ii. Kojoa mara kwa mara na hakikisha ni hadi mkojo unaisha ili kibofu kiwe tupu
iii. Kwa maumivu ya mlango wa mkojo, oga na kuosha kwa maji ya moto, kutapunguza maumivu

*Njia za Kujikinga na U.T.I*
Kunywa maji na vinywaji kwa wingi kila siku. Hii itakusaidia ukojoe mara kwa mara na kutoruhusu bacteria kujenga makazi kwenye njia ya mkojo
Kojoa kila ujisikiapo mkojo na usiubane kwa muda mrefu
Kwa wanawake
Nenda ukakojoe mara tu umalizapo tendo la kujamiiana. Hii itasaidia kutoruhusu bacteria kuingia na kujenga makazi kwenye njia ya mkojo.
Badili pedi mara kwa mara uwapo hedhini
Epuka kujisafisha ukeni na maji yarukayo kwa kasi, pia epuka kupilizia marashi ukeni, ama kutumia pedi zenye kemikali ya kukata harufu. Hizo huua bacteria wa asili wa ukeni hali ambayo hukaribisha bacteria wa maradhi kuzaliana kwa wingi
Ujisafishapo baada ya kujisaidia anzia mbele kwenda nyuma kuepusha kuhamisha bacteria walio eneo la haja kubwa kuingia njia ya mkojo
Kwa wale walio katika kipindi cha ukomo wa hedhi, wanaweza kushauliana na daktari juu ya kutumia oestrogen ya ukeni kuwasaidia kujikinga na maambukizi
Kwa wanaume
Kuhakikisha maeneo ya ncha ya uume ni masafi mara zote, hasa ikiwa hujatahiriwa kuepusha kujihifadhi na kuzaliana kwa vijidudu visababishao maradhi.
Kondom wakati wa kujamiiana nayo ni kinga nzuri

*Asanteni kwa kutenga muda wenu kupata elimu hii*

* _Dr. Brown Fm
MD*_

Comments

Popular posts from this blog

DAWA YA ASILI NA USAFI KWA WANAWAKE NI MUHIMU

Dawa ya Uchafu Ukeni Kwa kawaida mwanamke hutokwa na majimaji mepesi (vaginal fluids) yenye rangi nyeupe au ya njano. Inapotokea anatokwa na majimaji yenye ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali na muwasho, hiyo huwa ni ishara ya ugonjwa uitwao wa kutokwa uchafu ukeni ujulikanao kwa kitaalamu kama ‘Vaginosis’. Mwanamke mwenye tatizo hili hujisikia vibaya na anaweza akaacha kushiriki tendo la ndoa ama kwa kuhofia maumivu au kwa kuona aibu kwani mwanaume ni vigumu kuvumilia harufu hiyo au hata kuuona tu huo ute ute kwani humjengea hisia kwamba mwenza wake atakuwa na magonjwa ya zinaa au si mwaminifu kwa ujumla. Kinachosababisha kutokwa na uchafu ukeni: • Kuwa na wapenzi wengi • Baadhi ya dawa za uzazi wa mpango • Kusafisha uke kwa kutumia dawa zenye kemikali • Uchafu • Uvutaji sigara • Pombe • Maambukizi ya Bakteria au bakteria wabaya wanapozidi ukeni Dalili: • Kutokwa na uchafu us...

FAIDA ZA MAZIWA YA SOYA MWILINI

DONDOO ZA AFYA........!!!! MAAJABU YA SOYA MWILINI. MAAJABU YA SOYA MWILINI. Soya ni zao la jamii ya mikunde lenye aina nyingi za matumizi; ni zao linalofaa kwa chakula cha binadamu na wanyama na pia ni zao la biashara. Zao hilo lina kiasi kingi cha protini yenye ubora wa hali ya juu kuliko kiasi kilichopo katika aina nyingine ya mazao ya mimea.ZK  taasisi inayojishughuliza na uzalishaji wa bidhaa za vyakula lishe na mimea na matunda, vinavyoweza kutiba magonjwa mbalimbali wamezalisha maziwa ya Soya ambayo yana  kiasi cha protini inayozidi hata kiasi cha protini katika nyama, mayai na maziwa. Hii inamaanisha kuwa maziwa ya soya ni chanzo rahisi na cha bei nafuu cha protini hasa kwa watu wenye kipato kidogo ambao hawawezi kumudu gharama za vyanzo vingine vya protini kama nyama, maziwa na samaki. Aidha, maziwa ya soya yanaa mafuta bora yasiyo kuwa na lehemu (cholesterol). Uwingi na ubora wa protini katika maziwa ya soya yanaweza kuondoa utapiamlo hususani kwa watoto na kuwao...

FAIDA 30 ZA ALOE VERA MWILINI

FAIDA ZA MMEA WA ALOE VERA (Mshubiri): Mshubiri ni mti wenye Miujiza ya kutibu maradhi sugu kama ugonjwa wa Saratani (Cancer) ugonjwa wa Kisukari Diabetis, Ugonjwa wa cholesterol, ugonjwa wa kuvimba sehemu ya mwili na magonjwa mengine mengi. Tuone faida za mmea wa aloe vera au mshubiri 1. Huondoa uvimbe katika jicho Weka kiasi kidogo cha majimaji ya mu-aloe vera freshi kisha kuamka asubuhi, acha kwa dakika kadhaa kisha jisafishe. Uvimbe lazima ukimbie. Pia unaweza kuloweka pamba katika majimaji ya mualoe vera na kisha jisafishe katika jicho lenye uvimbe. 2. Huzuia na kuondoa michirizi ya tumbo itokanayo na ujauzito Anza kwa kupakaa majimaji ya mualoevera juu ya tumbo lako na ufanye kama masaji hivi taratibu juu ya tumbo mara 2 kwa siku katika kipindi chote cha ujauzito na baada ya kujifungua kwa miezi michache mpaka michirizi ipotee yote. 3. Hutibu bawasiri Ile ile sifa moja iliyonayo ya kutibu uvimbe ambayo inaweza pia kutibu malengelenge na uvimbeuchungu kwenye mwako wa mwili...