TAARIFA KWA UMMA Kuna taarifa za uzushi zinaenezwa za viongozi wanao tajwa kuwa ni viongozi wa CHADEMA Kata ya Ormelili na kwamba wamejiuzulu nafasi zao sio za kweli, Watu wanaotajwa sio viongozi wa CHADEMA na hawajawahi kuwa Viongozi wa CHADEMA wa Kata ya Ormelili. Aidha tunawataka CCM waache maaigizo ya kuwavalisha watu nguo zao na kuwapa vyeo kwa sifa za kisiasa. Kitendo cha kuwapachika watu sifa na vyeo vya kiuongozi visivyo vyao na kusema kuwa wamejiuzulu ni kosa la jinai (IMPERSONATION). Udanganyifu huu ni wa aibu na kamwe watu wa SIHA hawatayumba na sarakasi hizi na vituko hivi. Imetolewa na; Mozec Joseph Afisa-Habari na Mawasiliano CHADEMA Kanda ya Kaskazini. 28.01.2018
Usipitwe na Habari za Kila Kona ya Dunia.