Baada ya kipigo cha Azam FC, Simba wanaisubiri URA kujua hatma yao
January 6 2017 michuano ya Kombe laMapinduzi 2018 iliendelea kama kawaida visiwani Zanzibar kwa michezo kadhaa kuchezwa, mchezo kati ya Azam FC dhidi yaSimba SC ndio ulikuwa mchezo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka kwani timu hizo zimekuwa zipeana ushindani sana.
Simba walikuwa wanaingia uwanjani kucheza dhidi ya Azam FC inayohitaji matokeo ya ushindi ili kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali kwani matokeo tasa au kupoteza mchezo wangekuwa wametolewa katika michuano hiyo moja kwa moja.
Dhamira ya Azam FC kutinga hatua ya nusu fainali ilitimia dakika ya 59 baada ya Iddy Kipagwile kufunga goli ambalo hadi dakika 90 zinamalizika mchezo ulikuwa 1-0, Simba sasa atakuwa na wakati mgumu wa kuamua hatma yake kwa kupata ushindi mchezo wake wa mwisho dhidi ya URA ya Uganda, kwani sare itawatoa katika mashindano hayo.
Msimamo wa Kundi lao Azam FC anaongoza Kundi kwa kuwa na point tisa akifuatiwa na URA wenye point saba, Simba nafasi ya tatu kwa kuwa na point nne wakati timu za Mwenge na Jamhuri zimetolewa tayari lakini Simba watahitajika kupata matokeo ya ushindi dhidi ya URA katika mchezo wao wa mwisho.
Comments