Leo January 6, 2018 Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema umoja huo utachunguza shambulizi lililofanyika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo mwezi uliopita ambapo wanajeshi 15 wa kulinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania waliuawa.
Dmitry Titov, raia wa Urusi ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameteuliwa kuongoza uchunguzi wa mazingira yaliyolizunguka shambulizi hilo, kutathimini iwapo kikosi cha wanajeshi wa kulinda amani kilikuwa tayari kujihami dhidi ya mashambulizi na kutoa mapendekezo ya kuepusha mashambulizi zaidi..
Mbali na maafisa wa Umoja wa Mataifa kuhusika katika uchunguzi, maafisa wawili wa kijeshi kutoka Tanzania watajumuishwa katika kundi hilo la uchunguzi. Waasi wa kundi la Allied Democratic Forces ADF wanashukiwa kuhusika na shambulizi hilo.
Comments