Leo January 6, 2018 Baba mzazi wa nyota wa Barcelona Lionel Messi, Jorge Messi amezungumzia taarifa zinazosamba kuwa endapo jimbo la Catalonia litajitenga kutoka Hispania nyota huyo ataachana na klabu hiyo kuwa ni taarifa za uongo.
Jorge ameyasema hayo kwenye mahojiano na ‘Radio Red’ ya Argentina na kufafanua kuwa hakuna kipengele kinachotaka Messi aondoke Barcelona endapo Catalonia itajitenga na Hispania.
”Taarifa hizo ni za uongo, mkataba mpya wa Messi hauna kipengele hicho, ila tu kuna maelewano yanayotaka pande zote mbili kuzingatia, Barcelona ni timu kubwa na inawachezaji wakubwa kwa hiyo inatakiwa kucheza ligi kubwa haijalishi ni ligi gani ila iwe moja ya ligi kubwa”, – Jorge Messi
Comments