Ndege mbili za abiria zimegongana katika Uwanja wa Ndege wa Toronto nchini Canada usiku wa kuamkia leo January 6, 2016.
Inaelezwa kuwa hakuna vifo na majeruhi yuko mmoja tu ambaye aliwahishwa hospitali. Ndege moja ambayo ilikuwa na abiria 168 ambayo inaitwa Westjet iliyokuwa ikiwasili kutoka Cancun Mexico na ilipogongwa na Sunwing Aircraft ambayo haikuwa na abiria.
Baada ya ndege hizo kugongana moto mdogo uliwaka katika eneo hilo na ndipo abiria waliokuwa kwenye ndege ya Westjet walipoanza kutoka nje ya ndege hiyo kupitia mlango wa dharura hivyo kuepuka madhara zaidi ambayo yangeweza kuwapata.
Comments