Leo January 6, 2018 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Humphrey Polepole ametangaza uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi kumteua Maulid Mtulia kugombea ubunge jimbo la Kinondoni Dar es Salaam huku ikimteua Dr. Godwin Mollel kugombea kwenye jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro.
Wawili hawa walitangaza kujivua uanachama na nyadhifa zao zote za chama wiki chache zilizopita, Mtulia akiwa Mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CUF wakati Dr. Mollel akiwa Mbunge wa Siha kwa tiketi ya CHADEMA.
Taarifa zilizotolewa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole wa CCM na kueleza wagombea hao wafike katika mikoa husika yalipo majimbo yao ili kupokea maelekezo yanayohusu uchaguzi kutoka kwa makatibu wa CCM Jumanne ya January 9, 2018.
Comments