Skip to main content

Posts

Showing posts from May, 2018

Sheria ya kusajili blog yafutwa na Mahakama Kuu Kenya

Mahakama nchini kenya imetupilia mbali sheria mpya ya mitandao ya kutaka vyombo vya habari vya mitandao zikiemo blog kusajiliwa. Chama cha Wanablogu wa Kenya (BAKE) na Umoja wa Kenya wa Waandishi wa Habari (KUJ) kwa mafanikio waliomba rufaa kuzuia sheria hiyo   ambayo ilisainiwa  na Rais Uhuru Kenyatta wiki mbili zilizopita Jumanne, hakimu wa mahakama ya juu Chacha Mwita aliorodhesha vipengele 26 vya sheria hiyo   ambavyo vitaathiri haki na uhuru wa msingi wa kujieleza.  Mkurugenzi wa BAKE James Wamathai alisema: "vipengele hivi vinatakiwa kudhibiti habari za uwongo lakini kwa bahati mbaya hiyo ni kinyume na katiba ... kuna sheria zilizopo za kukabiliana na kesi wakati mtu amelala, hatuhitaji hili." Nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania   zimepitisha sheria ambazo wanaharakati wanalalamika kuzuia uhuru wa kujieleza. Mnamo Aprili, Uganda ilitangaza mipango ya kutoza kodi watumiaji wa vyombo vya habari vya mitandaoni.

Babu Tale Anakabiliwa na Kesi ya Madai ya Mil 250

Mkurugenzi wa Tip Top Connection Hamis Taletale a.k.a Babu Tale ameachiwa huru toka Kituo Kikuu cha Polisi DSM. Tale anakabiliwa na kesi ya madai ya fidia ya shilingi milioni 250 baada ya kushtakiwa kwa kosa la kutumia kazi ya Mhadhiri Sheikh Hashim Mbonde bila ridhaa yake. Kwa habari nyingine bonyeza hapa !

Breaking News! Mwanafunzi Muhimbili Akutwa Amekufa Chumbani Kwake

Hivi Punde: Mwanafunzi wa mwaka wa tatu Shahada ya Famasia katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Edward Kahitwa amekutwa akiwa amefariki chumbani kwake, chuoni hapo. Afisa Uhusiano wa chuo hicho, Hellen Mtui amethibitisha.

RC MAKONDA APOKEA VIFAA VYENYE THAMANI MILION 400 KWAAJILI YA UJENZI WA OFISI ZA WALIMU

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amekabidhiwa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi Million 400 kutoka kiwanda cha MMI Steel ltd kwaajili ya kampeni ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu Dar es salaam. Vifaa alivyokabidhiwa ni Mabati 15,000 yenye thamani ya shilingi Million 360, Nondo Tani 22 zenye thamani ya million 40 ambapo kiwanda hicho kimemuahidi tena kumpatia RC Makonda vifaa vingine ikiwemo Rangi, Nondo na Mabati. Akipokea vifaa hivyo RC Makonda ameshukuru kiwanda cha MMI Steel chini ya mkurugenzi wake Subhash Patel kwa kuwa mdau mkubwa wa kampeni ya ujenzi wa ofisi za walimu na kuwasihi wadau na wananchi kujitokeza kuchangia kampeni hiyo ili kutoa heshima kwa walimu. Aidha RC Makonda amesema kampeni ya ujezi wa ofisi za walimu inaendelea vizuri ambapo hivi karibuni atapokea kontena nyingine 16 za furniture kutoka Marekani, Kontena 10 za Vitabu kwaajili ya Maktaba ya jamii kutoka Marekani, Kontena 10 za vifaa tiba kutoka uingereza na kontena 10 za ...

Jimbo la Mbagala Kutenganishwa-Ofisi ya Rais TAMISEMI

Serikali kupitia Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeadhimilia kuligawa Jimbo la Mbagala lililopo jijini Dar es Salaam baada ya kuwepo kwa idadi kubwa ya wakazi wanaoishi jimboni humo na kusababisha uhaba wa upatikanaji wa huduma muhimu kutoka kwa Mbunge wao. Soma habari zingine hapa

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Ustawishaji Makao Makuu Apandishwa Kizimbani

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), Paskas Muragili na mwenzake mmoja wamepandishwa kizimbani kwa kutumia madaraka vibaya. Wanatuhumiwa kutokuweka wazi maslahi yao walipotoa zabuni ya TZS 86.1m kwa Glaciaer Investment

Serikali Imekanusha Kuhusiana Kuwakandamiza Haki za Wamasai Loliondo

Wizara ya Maliasili na Utalii imekanusha taarifa ya taasisi ya Oakland ya nchini Marekani kuwa, serikali ya Tanzania inadaiwa kukandamiza haki za Wamasai wanaoishi Loliondo. Imeeleza kuwa serikali imechukua hatua stahiki kutatua mgogoro katika eneo hilo na itatoa taarifa rasmi. Soma habari zingine kwa kina bonyeza hapa

Serikali imefuta leseni za wanaohodhi maeneo ya madini

Serikali imefuta leseni zote za kuhodhi maeneo ya madini na wamiliki wake kutakiwa kuomba upya wakizingatia sheria ya madini na kanuni zake. M/kiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula amesema, maeneo yote yaliyopewa leseni yanarejeshwa serikalini bila hakikisho la kupewa tena.

Rais wa Ghana Asimamishwa Kazi na Majaji

Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo amewasimamisha kazi majaji wanne wa mahakama kuu, baada ya kunaswa kwenye mkanda wa video wakipokea rushwa na mwingine akitaka rushwa ya ngono, ili kushinikiza uamuzi wa kesi.

France Chaos in Paris Opera knife attack, one man killed and 4 injured

One killed, 4 others injured in Paris knife attack: police The incident took place in Opera district of central Paris, and the site was about 400 meters away from Paris Opera House. PARIS - A man randomly attacked bystanders with a knife on Saturday night in central Paris, Paris prefecture confirmed. "Five people in the 2nd district of Paris were attacked by an individual armed with a knife," the prefecture tweeted. "One victim died. Two were seriously injured and two were wounded slightly," it added. The knife attacker, not identified yet, was shot dead by police. The incident took place in Opera district of central Paris, and the site was about 400 meters away from Paris Opera House. French Interior Minister Gerard Collomb denounced "heinous act" and praised police "composure" and swift reaction to neutralize the attacker. Citing a police source, French newspaper Le Figaro reported that the operating mode of the attacker, who shouted so...

R. Kelly has Accused for Sexually Abusing Minor, See What Next!

Photo by Michael Loccisano/Getty Images Spotify has announced that it will no longer promote the music of R. Kelly,  Billboard reports . Kelly’s music will remain available on the streaming service, but it won’t appear on any of the playlists that Spotify curates. The change comes under Spotify’s new  Hate Content & Hateful Conduct policy , which it developed in partnership with advocacy groups, including the Southern Poverty Law Center, the Anti-Defamation League, Color of Change, Showing Up for Racial Justice (SURJ), GLAAD, Muslim Advocates, and the International Network Against Cyber Hate. Under this new policy, Spotify says it will remove content that “expressly and principally promotes, advocates, or incites hatred or violence against a group or individual based on characteristics, including, race, religion, gender identity, sex, ethnicity, nationality, sexual orientation, veteran status, or disability.” Kelly’s music falls under the policy’s “hateful conduct by ...

Mzee wa Miaka zaidi ya 100 aomba kuuliwa kwa sindano ya sumu.

Kesho, madaktari wanatarajiwa kuweka sindano iliyojazwa dawa ya sodium pentobarbital katika mshipa wa Mwanasayansi huyo mkongwe duniani na kumuacha aisukume mwenyewe kwenda mwilini mwake. David Goodall amelazimika kusafiri kutoka Australia mpaka Basel, Uswisi kukifuata kifo baada ya sheria za kwao kutomruhusu kufanya hivyo. Akihojiwa na shirika la utangazaji la Marekani CNN, Goodall amesema maisha yake hayana thamani tena ndio maana ameamua kuomba kujiua akiamini hadithi yake itakuwa mfano na kuhamasisha uamuzi kama huo kwa wengine waliochoka kuishi. Katika mahojiano David Goodall amenukuliwa akisema " Natamani ningekuwa na uwezo wa kutembea mashambani na kuona vitu vinavyonizunguka. "Katika umri huu naamka asubuhi, nakunywa chai. Nasubiri mchana nile halafu sina cha kufanya tena. Maisha ya aina hii ya kazi gani? Goodall aliyezaliwa katika Jiji la London Aprili 1914, anatarajia kufa akiwa na miaka 104 ambapo ameweka wazi kuwa maisha yake yalisimama miak...

Ethiopia Watangaza kununua Bombardier Q400, 10

Shirika la Ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines), limetangaza kununua ndege 10 aina ya Bombadier Q400, kwa gharama ya USD 332 milioni, lengo likiwa ni kupanua soko lake barani Afrika. Ndege hizo zimelengwa kwenda katika maeneo ambayo viwanja vyake haviwezi kuhimili ndege kubwa.

TRA Mwanza Yaanza Kuwapatia Vitambulisho Wafanya biashara wadogo.

TRA Mkoa wa Mwanza imeanza kuwasajili wafanyabiashara wadogo na kuwapatia vitambulisho kwa gharama ya shilingi 10,000  kwa kila mmoja ndani ya miaka 3, lengo likiwa ni kuwatambua ili waweze kulipa kodi na kuondokana na adha ya kusumbuliwa kwenye maeneo wanayofanyia biashara. Kwa habari nyingine zaidi bonyeza hapa

Tuzo ya Fasihi ya Nobel Yasitisha Kutolewa, Fuatilia kwanini isitishwe?

Tuzo ya Fasihi ya #Nobel imesitishwa kutolewa kwa mwaka huu, kutokana na Taasisi ya Utamaduni ya Shule ya Mafunzo ya #Sweden inayohusika na utayarishaji wa tuzo hizo, kukumbwa na kashfa ya kimapenzi na uchumi. Kusitishwa huko hakutaathiri utoalewaji wa tuzo nyingine za Nobel. Kwa habari nyingine bonyeza kwenye maandishi haya ya bluu hapa

Safari ya Mwisho ya Wenger Dimbani kama Kocha

Arsene Wenger leo ataingia katika dimba la Arsenal (Emirates) kwa mara ya mwisho akiwa kocha wa timu hiyo. Wenger atastaafu mwishoni mwa msimu huu baada ya kuifundisha klabu hiyo kwa miaka 22. Arsenal iliyopo nafasi ya 6 leo itacheza dhidi ya Burnley.

Tanzania Yakataa Kudai Fidia kwa Utawala wa Wajerumani

Serikali ya Tanzania imekataa wito kutoka kwa wadau mbalimbali wakiitaka iidai Ujerumani fidia kutokana na uharibifu uliofanyika wakati ikiitawala, kati ya mwaka 1885 hadi 1918. Waziri Balozi Mahiga amesema, kuna njia bora kwa nchi hizo mbili kusaidiana, kuliko kudai fidia.

Burundi Yavifungia Vituo vya VOA na BBC

Burundi imevifungia kwa miezi 6 kuanzia Mei 7, 2018 vituo vya utangazaji, BBC na VOA kwa kukiuka sheria na kuvunja maadili ya utangazaji. Zuio hilo limekuja ikiwa zimebaki wiki 2 kabla ya kufanyika kura ya maoni zitakazomuwezesha Rais Nkurunziza kusalia madarakani hadi 2034.

Korea Kaskazini Yabadili Majira ya Saa, Angalia Sababu ya Kubadili Majira Hayo.

Korea Kaskazini imebadili muda wake (time zone), ili uendane na wa Korea Kusini ikiwa ni jitihada za kuchochea muungano kati ya nchi hizo mbili. Saa za Korea Kaskazini zilisogezwa mbele kwa dakika 30, baada ya kufanyika mkutano kati ya nchi hizo mbili wiki iliyopita. Wiki iliyopita marais hawa wawili walikutana na kuteta mambo ya kiusalama. Jambo la kukutana liliushangaza ulimwengu wote kwani walikuwa hawaelewani kabla kutokana na mizozo mbalimbali ya kiitikadi, na kiusalama zaidi.

Kanuni Nne Wanazotakiwa Waandishi wa Habari Wazifahamu

Four rules citizen journalists need to know Journalist training in Ethiopia (USAID) Technology and the reach of the internet have made it possible for citizen journalists to find large audiences. Although they don’t need print-distribution systems or the financial backing of a newspaper publisher, citizen journalists do need to know the principles good journalists have followed for decades. Anastasya Lloyd-Damnjanovic, who served as news editor for  The Daily Princetonian  and is currently a fellow at the the Woodrow Wilson International Center for Scholars, shares some imperatives for journalists to follow: Disclose conflicts of interest.  A potential conflict of interest is a reporter’s affiliation with the subject matter, source or media outlet. “Occasionally, I or another reporter got too close to our sources,” she explains. “At those times, editors found another reporter to interview the sources” or disclosed their conflicts of interest. Get both sides.  Rep...

Mlipuko Watokea Kisiwa cha Hawaii.

Wakazi 1,700 wakisiwa cha #Hawaii nchini Marekani, wamehamishwa kufuatia kulipuka kwa volcano kulikoambatana na tetemeko la ardhi katika mlima Kilauea. Hali ya hatari imetengazwa katika eneo hilo huku mamlaka zikiwataka wakazi hao kuchukua tahadhari kubwa. BBC

Mzigo wa mahindi wakatalia kichwani kwa mwizi

Mkazi wa Mbezi, Dar es salaam, Frank Japhet (23) amelazimika kujisalimisha kituo cha polisi Mlandizi, Kibaha, Pwani, baada ya mzigo wa mahindi unaokadiriwa kuwa na uzito wa kg 20, anaodaiwa kuuiba kung'ang'ania kichwani. Kwa maelezo ya mtuhumuwa huyo aliyoyatoa kituoni hapo, mzigo huo wa mahindi, uliofungwa kwenye kiroba aliuiba kwa mama mmoja eneo la mtaa wa Nyambwiro, Mlandizi, Kibaha, Pwani majira ya saa 7.00 usiku wa kuamkia leo. Amesema, alipoondoka na mzigo huo hadi eneo la stendi ya Mlandizi alipokuwa auache kwa mwenzake ili arudie mzigo mwingine, mzigo huo uling'ang'ania kichwani. Amesema, alijitahidi kufanya kila aliloweza ili mzigo huo utoke kichwani ikiwa ni pamoja na kulala ili akinyanyuka ubaki chini lakini aliponyanyuka, alinyanyuka nao kichwani! Baada ya kuzunguka nao kwa muda mrefu, alidai alichoka akalazimika kujisalimisha polisi ili asije akauawa na raia wenye hasira watakapobaini kuwa ni mwizi. Mpaka sasa yuko kituo cha polisi Mlandizi...

Mafuriko yaua watu 100

Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya limesema watu takribani ya 100 wamefariki kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini humo. Idadi ya watu ambao wameachwa bila makazi imekaribia robo milioni huku shirika hilo likitoa tahadhari kwamba huenda kukazuka magonjwa yanayoenezwa na maji machafu. Maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni Tana River na Garissa, ambapo Katibu Mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu Abbas Gullet, amesema, Idadi ya walioathirika inaendelea kupanda na kwamba hatua lazima zichukuliwe kwa haraka Amesema maeneo ya pwani na kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ndiyo yaliyoathiriwa zaidi ambapo kaya takriban 42,180 zimeachwa bila makao