Korea Kaskazini imebadili muda wake (time zone), ili uendane na wa Korea Kusini ikiwa ni jitihada za kuchochea muungano kati ya nchi hizo mbili.
Saa za Korea Kaskazini zilisogezwa mbele kwa dakika 30, baada ya kufanyika mkutano kati ya nchi hizo mbili wiki iliyopita.
Wiki iliyopita marais hawa wawili walikutana na kuteta mambo ya kiusalama. Jambo la kukutana liliushangaza ulimwengu wote kwani walikuwa hawaelewani kabla kutokana na mizozo mbalimbali ya kiitikadi, na kiusalama zaidi.
Comments