Skip to main content

Mzee wa Miaka zaidi ya 100 aomba kuuliwa kwa sindano ya sumu.

Kesho, madaktari wanatarajiwa kuweka sindano iliyojazwa dawa ya sodium pentobarbital katika mshipa wa Mwanasayansi huyo mkongwe duniani na kumuacha aisukume mwenyewe kwenda mwilini mwake.

David Goodall amelazimika kusafiri kutoka Australia mpaka Basel, Uswisi kukifuata kifo baada ya sheria za kwao kutomruhusu kufanya hivyo.


Akihojiwa na shirika la utangazaji la Marekani CNN, Goodall amesema maisha yake hayana thamani tena ndio maana ameamua kuomba kujiua akiamini hadithi yake itakuwa mfano na kuhamasisha uamuzi kama huo kwa wengine waliochoka kuishi.

Katika mahojiano David Goodall amenukuliwa akisema " Natamani ningekuwa na uwezo wa kutembea mashambani na kuona vitu vinavyonizunguka. "Katika umri huu naamka asubuhi, nakunywa chai. Nasubiri mchana nile halafu sina cha kufanya tena. Maisha ya aina hii ya kazi gani?

Goodall aliyezaliwa katika Jiji la London Aprili 1914, anatarajia kufa akiwa na miaka 104 ambapo ameweka wazi kuwa maisha yake yalisimama miaka 10 iliyopita baada ya kupoteza uoni na uwezo wa kutembea na alitamani kama kifo kingemchukua katika miaka hiyo

Comments

Popular posts from this blog

The court system during colonialism in Tanzania.

Introduction. Pre-colonial Period Administration of justice during this time depended heavily on the social economic and political organization of the society in Tanganyika. Two systems of administration of justice namely; The Centralized and the Non-Centralized systems could be identified at the time. The Centralized Systems was applicable to societies with chiefs who played both roles of adjudicators and that of governors. In the Non-Centralized systems the entire community took part in the adjudication of disputes. However in both systems there were no formalization of procedure in adjudication, the customs of the respective societies prevailed in the process. Colonial Period The German Colonial Period. The Land currently covering Tanzania Main Land, was then included in what was called the German East Africa, it was subjected to the German Colonial Rule from 1886 up to the end of the First Ward War, 1918. During this Germany Colonial Rule the Administration of Justi...

Ndege ya Ukraine yaanguka Iran ikiwa na abiria 180, Abiria wote wafariki

Ndege ya Ukraine aina ya Boeing-737 iliyokuwa na abiria 180 imeanguka Iran, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo. Watoa huduma wa msalaba mwekundu wa Iran wanasema kuwa hakuna dalili yeyote kama kuna mtu aliyepona katika ajali hiyo. Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la kimataifa la ndege la Ukraine ilianguka muda mfupi baada ya kuanza safari katika uwanja wa ndege wa Imam Khomeini mjini Tehran. Ripoti za awali zinadai kuwa ndege hiyo ilikuwa safarini kuelekea mji mkuu wa Ukraine, Kyiv.  Haijabainika ikiwa ajali hiyo ina uhusiano wowote na mzozo wa Iran-na Marekani. Kikosi cha uokoaji tayari kimetumwa katika eneo la tukio karibu na uwanja wa ndege, eneo ambalo ndege lilianguka. Credit: GettyImage " Ndege imeshika moto na tumetuma kikosi huko ... ," kiongozi wa huduma za dharura Pirhossein Koulivand,ameviambia vyombo vya habari ambapo Reuters imeripoti. Je tutegemee machafuko zaidi kutokea? Endelea kuwa pamoja nasi bega kwa bega, mshirikishe na mwenz...