Skip to main content

Posts

Ajali mbaya ya treni Uvinza Kigoma

Treni ya abiria imepata ajali mbaya . Treni ya abiria iliyokuwa ikisafiri kutoka Tabora kwenda Kigoma imeanguka mchana huu kati ya stesheni ya Malagarasi na Uvinza, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Ferdinand Mtui amethibitisha. Hadi sasa hakuna kifo kilichothibitishwa wala idadi ya majeruhi, kamanda huyo ameahidi kutoa taarifa zaidi baadaye baada ya kufika eneo la tukio. Kwa mujibu wa shuhuda wetu wa kulunzifikra blog  ajali hiyo imetokea mchana huu Februari 28, 2018, baada ya mabehewa mawili ya mbele na kichwa chake kuacha njia na kuanguka.

Namna ya kutunza nywele zenye mba

1. Kwanza kabisa unatakiwa kuosha nywele zako vizuri kwa kutumia shampoo ambayo imetengenezwa kwa ajili ya natural hair (nywele asili) au kama utatumia shampoo iliyotengenezwa kwa ajili ya nywele zenye dawa basi jaribu kutumia shampoo yenye conditioner. Hii itasaidia nywele zako kuwa laini na kuzuia zisiwe kavu baada ya kuziosha. 2. Pili ni kupaka mafuta nywele zako, zifanye nywele zako zivutie kwa kuzipaka mafuta ya maji kama vile mafuta ya nazi, olive oil, jojoba oil au castor oil kwasababu mafuta haya hulainisha ngozi ya kichwa, kufanya nywele zikue vizuri na kuzuia mba. Mafuta ya mgando hutengeneza mba kwenye nywele za asili kwa urahisi sana tofauti na nywele zenye dawa. 3. Pia usisahau kuzifanyia steaming nywele zako kwa mwezi hata mara 2, tumia steaming products kwa ajili ya natural hair au fanya steaming ya yai ni nzuri sana kwa kurutubisha nywele za asili. Osha nywele zako na shampoo kisha koroga yai na paka kichwani kwenye ngozi, Vaa kofia ya plastic kwa dakika 45, kisha osh...

Habari za Michezo Hizi Hapa

Mambo vipi watu wangu wa nguvu! Nakuletea highlight ya mchezo,wa jana kwa timu ya Man United dhidi ya Sevilla ambapo Man United walikuwa ugenini walipambana na kutoka kwa matokeo ya sare ya bila kufungana.  Mechi ya Shacter Donestc ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani iliwachapa FC Roma mabao mawili kwa moja 2:1 japo timu ya Roma walikuwa wa kwanza kupata goli lakini vijana wa Shacter waliongeza goli la pili katika mchezo huo. Angali ratiba ya mechi zijazo kwenye msimu huu wa La liga 2018