1. Kwanza kabisa unatakiwa kuosha nywele zako vizuri kwa kutumia shampoo ambayo imetengenezwa kwa ajili ya natural hair (nywele asili) au kama utatumia shampoo iliyotengenezwa kwa ajili ya nywele zenye dawa basi jaribu kutumia shampoo yenye conditioner. Hii itasaidia nywele zako kuwa laini na kuzuia zisiwe kavu baada ya kuziosha.
2. Pili ni kupaka mafuta nywele zako, zifanye nywele zako zivutie kwa kuzipaka mafuta ya maji kama vile mafuta ya nazi, olive oil, jojoba oil au castor oil kwasababu mafuta haya hulainisha ngozi ya kichwa, kufanya nywele zikue vizuri na kuzuia mba. Mafuta ya mgando hutengeneza mba kwenye nywele za asili kwa urahisi sana tofauti na nywele zenye dawa.
3. Pia usisahau kuzifanyia steaming nywele zako kwa mwezi hata mara 2, tumia steaming products kwa ajili ya natural hair au fanya steaming ya yai ni nzuri sana kwa kurutubisha nywele za asili. Osha nywele zako na shampoo kisha koroga yai na paka kichwani kwenye ngozi, Vaa kofia ya plastic kwa dakika 45, kisha osha vizuri.
4. Kitu kingine ni kuzichana vizuri nywele zako, nywele za kiafrika ambazo hazijawekwa dawa zina asili ya kujisokota au nyingine ni kipilipili hivyo mara nyingi huwa zinafungana, hivyo wakati wa kuchana inabidi uwe mwangalifu zisikatike, tumia chanuo ambalo ni pana na hakikisha umepaka hair lotion (hair moisturizer / pink lotion) kwenye nywele na mafuta ndio uanze kuchana taratibu. Wakati wa kulala jaribu kusuka mabutu na kuvaa kofia ili nywele zisijifunge au kujisokota.
Comments