KISA CHA MAREKANI UINGEREZA NA UFARANSA KUSHAMBULIA NCHINI SYRIA BILA YA IDHINI YA UMOJA WA MATAIFA.
Mapema 14 April 2018 Marekani Uingereza na Ufaransa zilifanya mashambulizi ya kijeshi nchini Syria zikitumia ndege za kivita. Habari toka vyombo mbalimbali vya habari vililipoti kuwa jumla ya makombora 103 yalivyatuliwa yakiwa yamelenga maeneo mbalimbali lakini makombora 71 yalinduguliwa angani na majeshi ya Syria kabla hayajagonga sehemu yaliyokuwa yamelengeshwa. Vifaa vya ulinzi vya anga vilivyotumika kuyadungua makombora yaliyokuwa yamerushwa na Ndege za Marakani na washirika wake ni Vifaa vya ulinzi wa anga vya Urusi aina S-200. Hata hivyo vifaa hivi vya S-200 ni vifaa vya nyuma sana kwani Urusi kwa sasa ina vifaa vingine bora zaidi ambavyo ni S-300 S-400 na S-500 ambavyo havikutumika kujikinga na mashambulizi haya ya Marekani Uingereza na Ufaransa nchini Syria.
Baada ya mashambulizi haya ambayo hayakuwa na madhara makubwa kutokana na makombora mengi kuripuliwa yakiwa hayajagonga sehemu yaliyokuwa yamelengeshwa na mengine kukosa shabaha Urusi imekitaja kitendo hivyo kama cha uharifu kwa Taifa huru la Syria.Eidha Urusi haijaamua kujibu mashambulizi haya kwa kile inachoamini Syria kwa sasa ni Salama baada ya Waasi Waliokuwa wakipewa silaha na nchi za magharibi kushindwa vita na kuondoka kwa magubaliano maalumu.
Urusi haijajibu mashambulizi kwa kujua nia ovu ya mataifa haya yanayotafuta kuona Syria ikiendelea kuwa sehemu ya vita hadi Rais wa nchi hiyo aondoke madarakani.
Urusi haijajibu mashambulizi kwa kuangalia maslahi mapana ya maisha ya watu wa Syria ambao wanahitaji mda wa kupumzika baada ya miaka 6 ya vita.
Urussi haijajibu mashambulizi hayo kwa kuangalia maslahi mapana ya kuepusha vita vya tatu vya dunia ambavyo vinaweza kuathiri maslahi ya Urussi hasa katika kipindi hiki ambacho miezi michache Mashindano ya kabumbu ya kombe la Dunia ambayo yataanza nchini Urusi hivi karibuni.
Kwa Upande wa Marekani Rais Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter kuwa "Kazi imekamilika" huku akiwapongeza washirika wake ambao ni Uingereza na Marekani.
Hata hivyo Rais Trump na Washirika wake wamepata upinzani mkali toka ndani na nje ya Marekani kwa mashambulizi hayo ambayo hayakuwa na kibali cha Umoja wa mataifa lakini pia yakionekana kama uonevu kwani hapakuwa na visibitisho vya wazi kama serikali ya Syria ilitumia silaha za kemikali kwa raia wake.Huku wachunguzi wa masuala ya kisiasa wakihoji kwa nini rais Bashar Al Assad atumie silaha za kemikali kwa watu wake huku vita vikiwa vimemalizika.
Kwa Upande wa gharama za mashambulizi hayo ya mda mfupi kizikadiliwa ni zaidi ya dollar za marekani $60,000,000 ikiwa gharama ya kombora moja ni zaidi ya dollar $500,000 pasipo gharama za mafuta ya ndege n.k
Comments