Wakati rais wa nchi ya Urusi Vladimr Putin akiwa anasisitiza kusimamishwa kwa mapigano angalau kwa saa 5 kila siku ili kutoa msaada kwa wanadamu wanaodhulika na vita kati ya wapiganaji wa Syria na wanamgambo wasiotaka suluhu. Lakini kuna maumivu yanayowapata wanadamu hasa watoto, wazee, na akina mama wasiojiweza kufanya lolote. Wiki hii luna kikao kilichokuwa kinaendelea ambacho walikiita 'HUMANITARIAN PAUSE' kwa ajili ya kupunguza mapigano kati ya waasi na wapiganaji wa majeshi ya Syria. Lakini bado vita hivi vinaacha majanga makubwa sana kwa maisha ya mwanadamu.
Dunia imeshtushwa na picha Hii ya kuhuzunisha ya kijana wa miaka Minne (4) ,aliyekuwa akihama kutoka Syria kwenda Jordan. Maofisa wa UNHCR walikutana naye akitembea kwa miguu peke yake jangwani kutoka Syria akielekea Jordan.
Kitu pekee alichokuwa amebeba ni mfuko wa plastic, maarufu Kama Rambo, ambamo ndani yake Mlikuwa na nguo za marehemu mama yake na dadake ambao waliuawa Syria.
Maofisa hao wa UN Walishindwa kujizuia hisia zao na kuanza kulia... Ni huzuni kubwa sana... Kwa wenye watoto wanaelewa mtoto wa miaka 4 anakuwaje...
Sasa fikiria kitoto hicho kinatembea jangwani peke yake.. Eee Mungu tunaomba amani. Vita visikie tu kwa jirani yako. Ni majonzi na simanzi kubwa isiyotaka hata kusahaurika.
Comments