NEEMA YA UPIMAJI AFYA BURE KWA WANA DAR ES SALAAM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam *Paul Makonda* anawatangazia Wananchi wote wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi kwenye Kampeni ya *Upimaji wa Afya Bure* kuanzia siku ya Jumatano ya *Septembe 06 -10* kwenye Viwanja vya *Mnazi Mmoja.*
Zoezi hilo litaendeshwa na *Madaktari bingwa* na *Wauguzi* zaidi ya *200* kutoka Hospital za *Umma, Jeshi na za Watu Binafsi* zilizomuunga mkono *RC Makonda.*
*Makonda* amesema kuwa hatopenda kuona Mwananchi anapoteza maisha kwa kukosa huduma ya Afya ndio maana ameamua kuendesha zoezi la upimaji wa *Afya Bure* ili Wananchi wapate fursa ya kujua Afya zao na kuwa na utaratibu wa kupima Afya zao mara kwa mara.
Aidha amezipongeza Hospital na zilizomuumga mkono ikiwemo *Muhimbili, Ocean Road, Amana, Temeke, Mwananyamala, Muhimbili, TMJ, Sanitas, Agha Khan, Regency, Kairuki, TANCDA, IMMI Life, APHTA, CCP Medicine, MDA, NHIF, Wandile wa kaya, P Consult, Besta Diagnestics, Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete, Jamii Bora na Damu salama.*
*Makonda* amesema watakaopimwa na kubainika kuwa na matatizo ya kiafya watapelekwa Hospital na kupatiwa *matibabu Bure*.
Hata hivyo amesema kuwa kutakuwepo na vifaa tiba vya kisasa, *Magari ya kubeba Wagonjwa,* Vyoo, Sehemu za watoa huduma na Sehemu za kupumzika wakati wa kusubiri huduma.
Comments