Skip to main content

HUKUMU YA KESI YA URAIS KENYA, YALIYOJIRI NI HAYA.

KESHO  IJUMAA NI  HUKUMU  YA KESI  YA  URAIS  KENYA, YALIYOJIRI  NI  HAYA.

Na Bashir  Yakub.
+255784482959.

1. WAHUSIKA

Walalamikaji(petitioners) ni wawili. Wa kwanza Raila Amolo Odinga na wa pili  Stephen Kalonzo Musyoka, mgombea mwenza.

Walalamikiwa(respondents) ni  watatu, wa kwanza ni tume huru ya uchaguzi IEBC. wa pili mwenyekiti wa tume hiyo ndg Wafula Chebukati na watatu ni ndg Uhuru Muigai Kenyatta.

Pia kuna walioomba kuingia katika kesi hiyo na kukubaliwa. Wa kwanza mwanasheria mkuu wa serikali ambaye ameingia kama rafiki wa mahakama(amicus curiae) , wa pili chama cha wanasheria kenya "Law Society of Kenya LSK," nao kama rafiki wa mahakama.

Wa tatu  na nne ni Dr Ekuru Aukot na Mr. Michael Wainaina ambao wameingia kama wahusika wenye maslahi(interested parties). Hawa nao walikuwa wagombea urais.

2. MUDA  WA KESI.

Kwa  katiba ya Kenya mlalamikaji anazo siku 7 tu za kufungua shauri tokea siku matokeo yalipotangazwa. Na mahakama inazo siku 14   tu za kusikiliza  na kutoa hukumu tokea siku shauri lilipofunguliwa.

Kesi  imekuwa ikisikilizwa hadi saa tano usiku  ikiwemo jumamosi na jumapili ili kuendana na muda wa katiba.

3. MAHAKAMA NA MAJAJI.

Mahakama inayosikiliza ni mahakama ya juu( the supreme court).

Majaji wanaosikiliza ni 7 wakiomgozwa na Jaji mkuu  David Maraga na naibu wake mwanamama Philomena Mwilu.

Wengine ni Jackton Ojwang, Mohammed Ibrahim, Njoki Ndung'u, Smokin Wanjala na Isaac Lenaola.

4. HOJA ZA MSINGI ZINAZOBISHANIWA.

(a) ODINGA : Hawa wanasema walishinda uchaguzi matokeo yakabadilishwa.
UHURU: Hawa wanasema matokeo yaliyotolewa yalikuwa halisi.

(b) ODINGA: Hawa wanasema mapungufu yaliyojitokeza yanatosha kubatilisha uchaguzi.
UHURU: Hawa wanasema ili mapungufu yabatilishe uchaguzi ni lazima mapungufu hayo yawe yameathiri  moja kwa moja namba/idadi ya kura.

(c) ODINGA: Hawa wanasema  server ya tume huru ikaguliwe kwa kuwa ilitumika kubadili matokeo.
UHURU: Hawa wanasema haiwezi kukaguliwa kwa kuwa ina code za siri ambazo zikijulikana zitaathiri chaguzi zijazo na usalama wa taifa.
 
(d)ODINGA : Hawa wanasema fomu nyingi za kukusanyia matokeo 34a, 34b na 34c  hazikutumwa kwa njia ya umeme kama inavyotakiwa na hivyo kuwa batili.
UHURU : Hawa wanasema sheria inasema njia ya umeme ikishindwa itumike manual hivyo baadhi ya maeneo njia hii ilifail na ikatumika manual.

(e) ODINGA : Hawa wanasema kiwango cha kuthibitisha kiwe ni Kulinganisha kinachowezekana zaidi(balance of probabilities) kwakuwa hili ni shauri la madai kama madai mengine.
UHURU: Hawa wanasema kiwango cha kuthibitisha kiwe "Pasi na Shaka" (beyond reasonable doubt).

(f) ODINGA: Hawa wanasema kuna matokeo yalianza kuingia sa 11 hata kabla vituo havijafungwa.
UHURU: Hawa wanasema kuna vituo vilikuwa na wapiga kura 20 au 50  hivyo wapiga kura waliisha, wakafunga mapema wakahesabu na kutuma.

(g) ODINGA: Hawa wanasema  baadhi ya fomu hazikusainiwa na kuwa na mihuri ya wasimamizi.
UHURU: Hawa wanasema uzembe wa wasimamizi hauwezi kufuta matakwa ya mpiga kura aliyesimama juani siku nzima.

(h) ODINGA:Hawa wanasema mwenyekiti alimtangaza mshindi hata kabla ya fomu zote kufika kutoka mashinani.
UHURU: Hawa wanasema  aliona hata akizisubiri haziwezi tena kubadili matokeo.

nk, nk, nk.

5. HUKUMU.

Hukumu itabeba jambo moja kati ya mawili. Ni kukubali ushindi wa Uhuru au kuubatilisha. Ikiubatilisha haitasema sasa Raila ndiye rais  bali itaamrisha uchaguzi wa rais kurudiwa.

Katiba inasema uchaguzi utarudiwa ndani ya siku 60 tokea siku ya hukumu.

6.  ATHARI  ZA HUKUMU.

Hukumu  itaathiri kesi zote za uchaguzi wa wabunge , seneta nk. zilizofunguliwa nchi nzima.

Kanuni zitakazochorwa na mahakama hiyo(jurisprudence) ndizo zitazotumika katika mahakama zote za chini kutoa maamuzi yake.

Kwahiyo ni hukumu yenye athari kubwa sana na  inayosubiriwa kwa hamu na gamu.

NI kesho  ijumaa tusubiri tuone.

Comments

Popular posts from this blog

DAWA YA ASILI NA USAFI KWA WANAWAKE NI MUHIMU

Dawa ya Uchafu Ukeni Kwa kawaida mwanamke hutokwa na majimaji mepesi (vaginal fluids) yenye rangi nyeupe au ya njano. Inapotokea anatokwa na majimaji yenye ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali na muwasho, hiyo huwa ni ishara ya ugonjwa uitwao wa kutokwa uchafu ukeni ujulikanao kwa kitaalamu kama ‘Vaginosis’. Mwanamke mwenye tatizo hili hujisikia vibaya na anaweza akaacha kushiriki tendo la ndoa ama kwa kuhofia maumivu au kwa kuona aibu kwani mwanaume ni vigumu kuvumilia harufu hiyo au hata kuuona tu huo ute ute kwani humjengea hisia kwamba mwenza wake atakuwa na magonjwa ya zinaa au si mwaminifu kwa ujumla. Kinachosababisha kutokwa na uchafu ukeni: • Kuwa na wapenzi wengi • Baadhi ya dawa za uzazi wa mpango • Kusafisha uke kwa kutumia dawa zenye kemikali • Uchafu • Uvutaji sigara • Pombe • Maambukizi ya Bakteria au bakteria wabaya wanapozidi ukeni Dalili: • Kutokwa na uchafu us...

FAIDA ZA MAZIWA YA SOYA MWILINI

DONDOO ZA AFYA........!!!! MAAJABU YA SOYA MWILINI. MAAJABU YA SOYA MWILINI. Soya ni zao la jamii ya mikunde lenye aina nyingi za matumizi; ni zao linalofaa kwa chakula cha binadamu na wanyama na pia ni zao la biashara. Zao hilo lina kiasi kingi cha protini yenye ubora wa hali ya juu kuliko kiasi kilichopo katika aina nyingine ya mazao ya mimea.ZK  taasisi inayojishughuliza na uzalishaji wa bidhaa za vyakula lishe na mimea na matunda, vinavyoweza kutiba magonjwa mbalimbali wamezalisha maziwa ya Soya ambayo yana  kiasi cha protini inayozidi hata kiasi cha protini katika nyama, mayai na maziwa. Hii inamaanisha kuwa maziwa ya soya ni chanzo rahisi na cha bei nafuu cha protini hasa kwa watu wenye kipato kidogo ambao hawawezi kumudu gharama za vyanzo vingine vya protini kama nyama, maziwa na samaki. Aidha, maziwa ya soya yanaa mafuta bora yasiyo kuwa na lehemu (cholesterol). Uwingi na ubora wa protini katika maziwa ya soya yanaweza kuondoa utapiamlo hususani kwa watoto na kuwao...

FAIDA 30 ZA ALOE VERA MWILINI

FAIDA ZA MMEA WA ALOE VERA (Mshubiri): Mshubiri ni mti wenye Miujiza ya kutibu maradhi sugu kama ugonjwa wa Saratani (Cancer) ugonjwa wa Kisukari Diabetis, Ugonjwa wa cholesterol, ugonjwa wa kuvimba sehemu ya mwili na magonjwa mengine mengi. Tuone faida za mmea wa aloe vera au mshubiri 1. Huondoa uvimbe katika jicho Weka kiasi kidogo cha majimaji ya mu-aloe vera freshi kisha kuamka asubuhi, acha kwa dakika kadhaa kisha jisafishe. Uvimbe lazima ukimbie. Pia unaweza kuloweka pamba katika majimaji ya mualoe vera na kisha jisafishe katika jicho lenye uvimbe. 2. Huzuia na kuondoa michirizi ya tumbo itokanayo na ujauzito Anza kwa kupakaa majimaji ya mualoevera juu ya tumbo lako na ufanye kama masaji hivi taratibu juu ya tumbo mara 2 kwa siku katika kipindi chote cha ujauzito na baada ya kujifungua kwa miezi michache mpaka michirizi ipotee yote. 3. Hutibu bawasiri Ile ile sifa moja iliyonayo ya kutibu uvimbe ambayo inaweza pia kutibu malengelenge na uvimbeuchungu kwenye mwako wa mwili...