Skip to main content

JE WAIFAHAMU HOMA YA INI NA MADHARA YAKE

*HEPATITIS(Homa ya ini)*

Hepatitis B ni maambukizi mabaya sana ya kirusi aitwaye hepatitis B virus (HBV) kwenye  maini. Kwa watu wengine ugonjwa huu huweza kuchukua zaidi ya miezi 6 (chronic). Ugonjwa huu ukichukua muda mrefu unaweza kuleta madhara ya kufeli kwa ini, kansa ya ini au liver cirrhosis hali ambayo itaacha makovu ya kudumu kwenye maini. Watu wengi wanaougua ugonjwa huu hupona kabisa.
Kuna chanjo ya kusaidia kuzuia hepatitis B lakini hakuna tiba pale ambapo tayari utakuwa umeambukizwa virusi wa hepatitis B. Ukishaambukizwa yafaa kuchukua tahadhari za kusaidia kutowaambukiza watu wengine.

*Dalili Za Hepatitis B*

Dalili za hepatitis B huanza kuonekana baada ya mwezi mmoja hadi minne baada ya kupata maambukizi, nazo ni:
. Maumivu ya tumbo
. Mkojo mweusi
. Homa
. Maumivu ya joints
. Kukosa hamu ya kula
. Kichefuchefu na kutapika
. Udhaifu wa mwili na mwili kukosa nguvu
. Macho na ngozi kugeuka rangi na kuwa vya njano

*Chanzo Cha Hepatitis B*
Ugomjwa wa hepatitis B husababishwa na kirusi aitwaye Hepatitis B virus (HBV). Kirusi huyu huambukizwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine kupitia damu, shahawa na maji maji mengine ya mwilini.

Njia kuu za uambukizaji zikiwa:
. Kujamiiana. Unaweza kuambukizwa na mtu mwenye ugonjwa huo kama utajamiiana naye bila kutumia kinga na damu, mate, shahawa au maji maji ya ukeni yakaingia ndani ya mwili wako.
. Kuchangia sindano. Kirusi wa hepatitis B anaambukiza kirahisi sana kupitia sindano zenye damu ya mtu mwenye virusi hivi.
. Mama kumwambukiza mtoto. Mama mwenye mimba mwenye virusi vya HBV anaweza kumwambukiza kichanga wakati wa tendo la uzazi. Mtoto anaweza kupewa chanjo baada ya kuzaliwa na akaepuka kuambukizwa, hivyo ni vizuri kuchukua tahadhari ya kujipima wakati una ujauzito.

Hepatitis B hugawanywa katika makundi mawili; Hepatitis ya muda mfupi (acute hepatitis) na hepatitis ya muda mrefu (chronic hepatitis).

Acute hepatitis B: Hii huchukua chini ya miezi 6 kupona. Kinga zako za mwili zinaweza kupambana na kuuondoa ugonjwa huu na ukapona kabisa katika muda mfupi. Watu wazima mara nyingi huugua acute hepatitis ingawa mara chache huweza kufikia kuwa chronic hepatitis.

Chronic hepatitis B: Ugonjwa huu huchukua miezi 6 au zaidi kupona. Kama kinga za mwili wako hazitaweza kuushinda, basi ugonjwa utakuwa ni wa maisha kwako na uwezekano wa maganjwa makubwa zaidi kama ya cirrhosis na saratani ya ini ukiongezeka. Chronic hepatitis B inaweza isigundulike kwa miaka mingi hadi mgonjwa atakapokuwa mahututi kutokana na ugonjwa huu wa homa ya ini.

*Madhara ya hepatitis B*
Kuwa na hepatitis B kwa muda mrefu (chronic hepatits) kunaweza kusababisha madhara makubwa yafutayo;
. Makovu kwenye ini (Cirrhosis). Kuvimba kwa ini kwa muda mrefu kunakotokana na virusi wa hepatitis B kunaweza kusababaisha makovu kwenye ini (cirrhosis) na kulifanya ini lishindwe kufanya kazi yake inavyotakiwa.
. Saratani ya ini. Watu wenye hapatitis B kwa muda mrefu wanaweza baadaye wakapata saratani ya ini.
. Ini kufeli. Ini likishindwa kufanya kazi zake kabisa, hatua nyingine ya kuwekewa ini jingine itahitajika.
. Matatizo mengine. Mgonjwa mwenye hepatitis B anaweza kupata matatizo ya figo, uvimbe kwenye mishipa ya damu na upungufu wa damu.
Tiba Ya Hepatitis B
Kama vipimo vikionyesha kuwa una hepatitis B ya muda mfupi (acute hepatitis), huhitaji tiba kwa sababu itaondoka yenyewe baada ya muda mfupi. Badala yake unahitaji kupumzika, kupata lishe bora na vinywaji vya kutosha wakati kinga zako za mwili zikipambana kuundoa ugonjwa huo.

*Dawa ya kutibu homa ya ini*

yaani zaidi ya miezi sita, utahitaj tiba ili kuondoa madhara ya ugonjwa huo na kuzuia usiwaambukize watu wengine.

Baadhiya tiba ni:
. Dawa za kuua virusi (antiviral medications) . Kuna dawa nyingi za kuweza kuua virusi ikiwa ni pamoja na lamivudine (Epivir), adefovir (Hepsera), telbivudine (Tyzeka) na entecavir (Baraclude).
. Interferon alfa-2b (Intron A). Hii hutolewa kama sindano na hasa hutumika kwa vijana wadogo au wanaotegemea kupata ujauzito. Madhara ya tiba hii ni kupata mfadhaiko, kubanwa kifua na kupumua kwa shida.
. Kubadilishiwa Maini. Kama maini yako yameharibika kabisa, upasuaji hufanyika na kuwekewa maini mengine.
   *xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx*

*Dr. Brown Fm*

Comments

Popular posts from this blog

DAWA YA ASILI NA USAFI KWA WANAWAKE NI MUHIMU

Dawa ya Uchafu Ukeni Kwa kawaida mwanamke hutokwa na majimaji mepesi (vaginal fluids) yenye rangi nyeupe au ya njano. Inapotokea anatokwa na majimaji yenye ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali na muwasho, hiyo huwa ni ishara ya ugonjwa uitwao wa kutokwa uchafu ukeni ujulikanao kwa kitaalamu kama ‘Vaginosis’. Mwanamke mwenye tatizo hili hujisikia vibaya na anaweza akaacha kushiriki tendo la ndoa ama kwa kuhofia maumivu au kwa kuona aibu kwani mwanaume ni vigumu kuvumilia harufu hiyo au hata kuuona tu huo ute ute kwani humjengea hisia kwamba mwenza wake atakuwa na magonjwa ya zinaa au si mwaminifu kwa ujumla. Kinachosababisha kutokwa na uchafu ukeni: • Kuwa na wapenzi wengi • Baadhi ya dawa za uzazi wa mpango • Kusafisha uke kwa kutumia dawa zenye kemikali • Uchafu • Uvutaji sigara • Pombe • Maambukizi ya Bakteria au bakteria wabaya wanapozidi ukeni Dalili: • Kutokwa na uchafu us...

FAIDA ZA MAZIWA YA SOYA MWILINI

DONDOO ZA AFYA........!!!! MAAJABU YA SOYA MWILINI. MAAJABU YA SOYA MWILINI. Soya ni zao la jamii ya mikunde lenye aina nyingi za matumizi; ni zao linalofaa kwa chakula cha binadamu na wanyama na pia ni zao la biashara. Zao hilo lina kiasi kingi cha protini yenye ubora wa hali ya juu kuliko kiasi kilichopo katika aina nyingine ya mazao ya mimea.ZK  taasisi inayojishughuliza na uzalishaji wa bidhaa za vyakula lishe na mimea na matunda, vinavyoweza kutiba magonjwa mbalimbali wamezalisha maziwa ya Soya ambayo yana  kiasi cha protini inayozidi hata kiasi cha protini katika nyama, mayai na maziwa. Hii inamaanisha kuwa maziwa ya soya ni chanzo rahisi na cha bei nafuu cha protini hasa kwa watu wenye kipato kidogo ambao hawawezi kumudu gharama za vyanzo vingine vya protini kama nyama, maziwa na samaki. Aidha, maziwa ya soya yanaa mafuta bora yasiyo kuwa na lehemu (cholesterol). Uwingi na ubora wa protini katika maziwa ya soya yanaweza kuondoa utapiamlo hususani kwa watoto na kuwao...

The court system during colonialism in Tanzania.

Introduction. Pre-colonial Period Administration of justice during this time depended heavily on the social economic and political organization of the society in Tanganyika. Two systems of administration of justice namely; The Centralized and the Non-Centralized systems could be identified at the time. The Centralized Systems was applicable to societies with chiefs who played both roles of adjudicators and that of governors. In the Non-Centralized systems the entire community took part in the adjudication of disputes. However in both systems there were no formalization of procedure in adjudication, the customs of the respective societies prevailed in the process. Colonial Period The German Colonial Period. The Land currently covering Tanzania Main Land, was then included in what was called the German East Africa, it was subjected to the German Colonial Rule from 1886 up to the end of the First Ward War, 1918. During this Germany Colonial Rule the Administration of Justi...