Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John P Magufuli ametokwa na machozi baada ya kuona majeneza ya miili ya watoto waliofariki wa shule ya Lucky Vicent walipokuwa wakiagwa kwenye uwanja wa Shehk Amri Abeid Arusha na kusema
"Nimepatwa na uchungu na majonzi makubwa ninapoyaona majeneza ya watoto na walezi wao waliopoteza maisha katika ajali ya basi huko Arusha, tumewapoteza mashujaa wetu katika elimu. Tuwaombee na tuendelee kuwa na subira, uvumilivu na ustahimilivu, tunapoomboleza vifo vya wapendwa wetu tuendelee kuwa wamoja. Mungu ibariki Tanzania" alisema Rais Magufuli Rais wa Tanzania alitoa machozi jana alipoona majeneza ya Marehemu huko Arusha
Comments